LIWALE YAIBUKA KIDEDEA KATIKA MASHINDANO YA UMISETA MKOA WA LINDI.
Halmashauri ya wilaya ya Liwale ilishiriki mashindano ya UMISETA yaliofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Lindi na Msinjairi. Mashindano hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Godfrey W. Zambi tarehe 29/05/2019 na kufungwa mnamo tarehe 01/06/2019 na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Mhe. Rehema Madenge.
Halmashauri ya Wilaya ya Liwale iliwakilishwa na timu ya watu 66, wakiwemo wanafunzi 60 na Walimu 6 ambao walishiriki katika michezo ya Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Riadha na Mpira wa Mikono na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Mpira wa Mikono kwa Timu ya wanaume. Aidha pia wanafunzi 13 na mwalimu 1 kutoka Halmashauri ya Wilaya Liwale walichaguliwa kati ya wanafunzi 100 waliounda timu ya Mkoa wa Mkoa wa Lindi inayokwenda shiriki mashindano ya UMISETA Kitaifa.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. Box 23 Liwale
Simu ya Mezani: +255 (0) 737 187 605
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2018 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.