WAKUU NA MAKAMU WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI LIWALE WANEEMEKA NA WARSA YA UONGOZI, UTAWALA NA UENDESHAJI WA SHULE NA TAASISI.
Akifungua warsha ya siku moja ilioandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale na kufanyika katika ukumbi wa kituo cha walimu Liwale (TRC) tarehe 26 Julai, 2019 Katibu Tawala Wilaya Ndg. Mbwana Kambangwa aliwasihi wajumbe kutumia warsa hii ambayo itawajengea uwezo wa kutatua changamoto za kiuongozi, utawala na uendeshaji wa shule za sekondari wilayani hapa, lakini pia aliwataka wakuu na makumu wakuu wa shule kutambua dhamana waliopewa, kuwajibika, kutatua migogoro, kuwa waadilifu na wabunifu katika maeneo yao ya kazi ili kuwajengea uwezo wanafunzi, kuongeza kiwango cha ufaulu katika ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa kwa ujumla.
Ikumbukwe kwamba Mkoa wa Lindi; uliibuka kinara kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2019 lakini umekuwa na matokeo yasioridhisha katika matokeo ya kidato cha nne, Katibu Tawala Wilaya ya Liwale Ndg. Mbwana Kambangwa alitumia nafasi hii pia kuwaomba wakuu wa shule za sekondari kuongeza nguvu na juhudi za kipekee ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika matokeo ya kidato cha nne.
Awali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Bernard H. Kivamba aliwapongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale kwa kushirikiana na Ofisi ya Elimu wilaya kwa kuaanda warsa hii muhimu katika kuwajengea uwezo wakuu na makumu wakuu wa shule za sekondari wilayani Liwale.
Warsha hii iliendeshwa na Dr. Lameck kutoka Chuo kikuo cha Dar es Salaam ambae aliwajengea uwezo kupitia mada mbalimbali zikiwemo uongozi na utawala bora, uendeshaji, uajibikaji, uzalendo, ubunifu, kutambua majukumu na mchango wao katika jamii. Wajumbe wa warsha hii walimshukuru Mkuu wa wilaya Mhe. Sarah Chiwamba kwa kuwaandalia warsha hii muhimu na yenye tija kwao na kuahidi kwenda kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao ya kazi na sekta ya elimu wilayani Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.