VIVUTIO VYA KIUTAMADUNI
MAENEO YA KIHISTORIA WILAYANI LIWALE
Na.
|
ENEO LA KIHISTORIA
|
MAHALI LILIPO
|
UMBALI
|
MAELEZO YA ENEO LA KIHISTORIA
|
1
|
Kituo cha misafara ya ngende
|
Kijiji cha ndapata
|
Km 80
|
Ni sehemu ambapo misafara ya kwenda ngende huanzia (kwenda Ilonga Mkoani Morogoro). Misafara hii hufanyika mara mbili kwa mwaka.
|
2
|
Kaburi la Mwindaji maarufu
|
Katika hifadhi ya msitu wa Selous
|
- |
Ni mwindaji wa Kizungu aliyejulikana kwa jina la Constantin John Philip Ionides, maarufu kwa jina la Mpalangozi ambaye alizaliwa tarehe 17/01/1901 na kufa tarehe 22/09/1968. Kaburi hili linapatikana karibu na mlima Nandanga.
|
3
|
Miti iliyobadilika kuwa mawe
|
Katika hifadhi ya msitu wa Selous
|
- |
Mawe haya yanapatikana eneo la makutano ya mito Njenje na Mbarang’andu.
|
4
|
Hifadhi ya Selous
|
Katika hifadhi ya msitu wa Selous
|
- |
Ni hifadhi ya pili kwa ukubwa duniani baada ya hifadhi ya Yellostone iliyoko Marekani.
Selous ilianzishwa mwaka 1896 na Wajerumani ikiwa na ukubwa wa KM za mraba 50,000. KM za mraba 25,335 zinapatikana Mkoa wa Lindi hasa Wilayani Liwale. Hifadhi hii inawanyamapori wengi wa aina mbalimbali. |
5
|
Mnara wa mashujaa
|
Kijiji cha mpirani
|
Km 1
|
Eneo walilonyongwa mashujaa wa kingindo waliokataa kutawaliwa na wakoloni wa kijerumani mwaka1905.
|
6
|
Mikukuyumbu
|
Kijiji cha kimambi
|
Km 52
|
Mahali alipoiwawa kiongozi wa dini wa dhehebu la Roman Catholi (Cassian Spiess) tarehe 14/08/1905, katiak harakati za kueneza dini ya Kikristo.
|
7
|
Kichuguu cha Mwl. Nyerere
|
Kijiji cha Mpigamiti
|
Km 40
|
Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere alisimama mwaka 1976, akiwa anakagua mashamba ya ushirika na kuongea na wananchi wa Mpigamiti.
|
8
|
Eneo la shabaha
|
Kijiji cha chimbuko
|
Km 40
|
Lilitumika na Wajerumani kufanyia mazoezi ya kulenga shabaha na linatumika hadi leo wakati wa mafunzo ya askari wa Jeshi la akiba.
|
9
|
Makaburi ya Wajerumani
|
Kijiji cha chimbuko
|
Km 40
|
Mabakuri haya ni ya karne ya 18.
|
10
|
Mlima Mwekundu
|
Kijiji cha ndapata
|
Km 80
|
Mlima huu ulimeguka na sehemu ya mlima iliyobaki ni nyekundu, wakati wa usiku sehemu hiyo uonekana kama inawaka moto.
|
11
|
Mlima nanungu
|
Katikati ya kijiji cha mpengere na mlembwe
|
Km 45
|
Kuna pango kubwa lenye kuku, njiwa na mbuzi ambao wanaishi humo bila kufugwa na mtu. Ni sehemu ya kufanyia matambiko.
|
12
|
Boma la zamani
|
Kijiji cha makonjiganga
|
Km 1
|
Lilijengwa na wakoloni wa kijerumani mwaka 1905, kwa ajili ya shughuli za utawala.
|
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.