Kata ya Barikiwa
|
|
|
Mh. Hemedi J. Libihi
|
|
|
Diwani Kata ya Barikiwa
|
TAARIFA YA KATA YA BARIKIWA ROBO YA KWANZA JULAI - SEPTEMBA 2017
|
|
|
Diwani wa Kata ya Barikiwa aliwasilisha taarifa ya utekelezaji katika Kata ya Barikiwa kipindi cha robo ya kwanza (Julai- Septemba, 2017). Katika Kata hiyo Baraza lilipokea:- taarifa ya idadi ya watu, taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, taarifa ya mapato na matumizi, taarifa ya maendeleo ya elimu sekondari na msingi, hali ya majanga, hali ya maendeleo ya kilimo, mifugo na uvuvi, Uzalendo,Utunzaji wa mazingira , hali ya Ulinzi na Usalama na Utawala bora,Maendeleo ya Afya, mafanikio yaliyopo na changamoto zilizojitokeza. Taarifa ilipokelewa. Katika kujadili taarifa hiyo wajumbe walisisitiza kuwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji (W) wajitahidi kutembelea vijijini na kuona changamoto za Wananchi. Aidha hoja ya upungufu wa walimu ilielezwa kuwa utaangaliwa uwezekano wa kupata walimu kwa vile Halmashauri imeomba vibali vya ajira. |
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.