Friday 14th, November 2025
@SHULE YA SEKONDARI YA KUTWA LIWALE NA SHULE YA SEKONDARI YA KIBUTUKA

Makarani waongoza wapiga kura wa Jimbo la Liwale, mkoani Lindi, wamekula kiapo cha kutunza siri na kutokuwa wanachama wa chama chochote cha siasa kama sehemu ya maandalizi ya kuanza kutekeleza majukumu yao katika Uchaguzi Mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Kiapo hicho kimetolewa leo Oktoba 25, 2025, kabla ya kuanza kwa mafunzo maalumu ya siku moja kwa makarani hao yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari ya Kutwa Liwale (Liwale Day) pamoja na Shule ya Sekondari Kibutuka.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Liwale, Bw. Winfrid Tamba, amewataka makarani hao kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), na kuepuka kupokea maelekezo kutoka kwa mamlaka nyingine zisizo na wajibu wa kisheria katika mchakato wa uchaguzi.
Aidha, Bw. Tamba amewataka makarani hao kuwa waadilifu, kutunza siri za kazi na kuhakikisha hawawi chanzo cha malalamiko au vurugu kutoka kwa wadau wa uchaguzi, hususan vyama vya siasa. Amewahimiza pia kutumia lugha yenye staha na weledi wakati wa kuwaongoza wapiga kura, ili kuhakikisha zoezi la kupiga kura linafanyika katika mazingira ya amani, utulivu na uwazi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.