Thursday 21st, November 2024
@
Kaimu Mratibu wa TASAF Wilaya ya Liwale Bi, Frola Mosha amesema Mpango wa TASAF awamu ya 4 na zoezi la tathmini kwa walengwa awamu ya pili na ugawaji wa ruzuku kwa walengwa umeanza na unaendelea katika Vijiji na Kata kwa Wilaya mzima.
Kwasasa TASAF Wilaya ya Liwale kama miongoni mwa maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunususru Kaya Masikini Awamu ya Pili unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania(TASAF) imefanya zoezi la uhawilishaji wa Ruzuku kwa Walengwa wa Mpango katika dirisha la Malipo lililofunguliwa tarehe 15-08.2023 mpaka tarehe 26.08.2023,Katika dirisha hili la malipo walengwa wamepewa ruzuku za malipo ya Mach-Aprili 2023 na Mei-Juni 2023 ambapo Walengwa wa Mpango wamelipwa malimbikizo yao yote ya Ujira wa Ajira za muda walizoshiriki katika mwaka wa 2022-2023 pamoja na ruzuku zingine ikiwamo,ruzuku za msgingi,ulemavu,na masharti ya elimu na afya,Aidha sambamba na malipo ya ruzuku dirisha hili la malipo limeambatana na zoezi la tathmini kwa walengwa kwa Vijiji 46 vya awali ambao walishindwa kufanyiwa tahmini mwezi Machi kutokana nasababu mbalimbali zilizowafanya washindwe kuhudhuria katika zoezi la tathmini aawamu ya kwanza.
Hata ivyo Tasaf Wilaya ya Liwale inaendelea kutoa Elimu kwa wanufaika kuwa na uelewa juu ya Mpango wa kunusuru kaya Masikini kupita walengwa, vipeperushi, pamoja na vyombo vya habari na kuwakumbusha TASAF ni nini ili wananchi wapate uelewa juu ya ufanyaji kazi mbalimbali, ufugaji, na kuwepo kwenye vikundi vya kuweka akiba kuwevitakavyo wasaidia kujikwamua kiuchumi.
Sambamba na zoezi la tathmini linaloendelea TASAF imefanikiwa kuwafikia walengwa wengi na kuwapa Elimu ambayo inayotolewa na wawezeshaji wakati wa warsha za kijamii zinazotolewa kwenye Vijiji wakati wa malipo na kuwasaidia urahisi wa upatikanaji wa huduma za Afya, Elimu, na Barabara katika Vijiji.
Aidha walengwa walio fikiwa na mpango wa kunusuru kaya masikini wameishukuru TASAF kwa kuwafikia na kuwasaidai katika kujikwamua na Umasikini kama ambavyo Malengo ya Mfuko huu ulivyo lakini pia Bi Zena Issa Chamoto ambaye ni mlengwa ameiomba kutatua changamoto wanazozipata ikiwemo Ujira, ufanyaji wa kazi utoaji wa Eimu na pia wameomba malipo kufanyika kwa wakati na kufuata kalenda ya malipo.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.