Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga ametembela Kata ya Mbaya katika Chama Cha Msingi cha Nduruka Amcos na Nambana Amcos ili kuangalia na kufatilia ugawaji wa pembejeo za ruzuku katika zao la korosho.
Mheshimiwa Mlinga amewataka wasimamizi ambao wanagawa pembejeo hizo kuhakikisha wakulima wote ambao wamejisajili wanapata pembejeo kwa wakati ili waweze kuhudumia mikorosho yao ambayo kwa sasa ndio msimu umeanza.
Hata hivyo Mheshimiwa Mlinga amewasisitiza wakulima kuendelea kuwa karibu na Maafisa ugani katika Kata zote ili waweze kupata taarifa za pembejeo ambazo zinaendelea kuingia na kugawiwa na pia changamoto zote ambazo zinatokana na mtandao zishulikiwe ili kumuondelea mkulima usumbufu.
Aidha katika kukagua na kufatilia ugawaji wa pembejeo Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amewataka wananchi wote wa Kata ya Mbaya wanajitokeza na kujiandikisha katika daftari la kudumu la Mpiga kura ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika chaguzi zijazo ikiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unakuja hivi karibuni.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.