Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amewataka wavunaji wote kufuata taratibu na sheria ambazo zipo na kuacha kuvuna kiamazoe ambao ni uvunaji haramu bali wafuate taraibu zilizopo hii imebainika kuwa viwanda vingi vinachakata magogo ambayo hayajakaguliwa na kugongwa jambo linalo sababisha Serikali kupoteza mapato yatokanayo na misitu katika Wilaya ya Liwale.
Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa” kumekuwa na uvunaji haramu ndani ya Wilaya ya Liwale wavunaji wengi wanavuna bila kufuata utaratibu wamekuwa wakivuna magogo na kusafirisha nyakati za usiku ili kukwepa kulipa tozo za Halmashauri na Wakala wa misitu Tanzania hii haikubaliki ni lazima kila mvunaji alipe” tozo zote ili kuendelea na uvunaji.
Mheshimiwa Mlinga katika oparesheni yake aliyoifanya kwenye Kata ya Mihumo amekamata jumla ya magogo 67 ambayo hayajakaguliwa wala kugongwa katika kiwanda cha ABG ya kiwa tiyari kwa ajili ya kuchakatwa hivyo ameagiza kusimamishwa kwa kiwanda na uchunguzi ufanyike mara moja.
Aidha Mheshimiwa Mlinga amewataka wavunaji wote waliopo kwenye Wilaya ya Liwale kuhakikisha wanafuata sheria na kuacha maramoja shughuli za uvunaji haramu na kusafirisha magogo kinyemela kwani kufanya hivyo ni kosa na pia kunaipotezea Serikali mapato na pia kila mvunaji atumie leseni yake na kuvuna katika sehemu aliyopewa bila kuzidisha na pia hakuna kutumia leseni ya mtu mwingine katika uvunaji ,hata hivyo amewataka wafanyabiashara kuwa wadilifu kwa kuacha kuwarubuni kamati za maliasili za vijiji kwa kuwapa rushwa ili wapate maeneo ya uvunaji.
Picha za magogo ambayo yamevunwa kinyemela yakiwa kiwandani kwa ajili ya uchakataji ambayo Mkuu wa Wilaya ya Liwale ameyakamata katika oparesheni yake.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.