Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amekutana na wadau mbalimbali wa elimu katika kikao cha utathimini na kujadili uripoti wa wanafunzi ambao wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na uwandikishwaji wa darasa la kwanza na wanafunzi ambao wameacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo wazazi kushindwa kusimamia watoto wao na utoro.
Katika kikao hicho kilihudhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Maafisa Elimu wa Wilaya, Watendaji wa Vijiji na Kata, Polisi Kata Walimu wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari Viongozi wa Chama na Viongozi wa Dini.
Mheshimiwa Mlinga amewataka wadau wote wa elimu katika Wilaya ya Liwale kuhakikisha kila mtu anatekeleza majukumu yake katika eneo lake ikiwemo kusimamia watoto wote ambao wamechaguliwa kuripoti shule ikiwemo kuwatafuta waliko na piwa wazazi wao kutafutwa walipo ili kushirikiana watoto wote waripoti shuleni.
Aidha Mheshimiwa Mlinga ametoa maagizo kwa vijiji vyote ambavyo vina mapato makubwa vihakikishe kuwa vinawasidia wanafunzi ambao hawana uwezo wa kupata mahitaji kwa kuwapatia mahitaji muhimu kwa ajili ya shule ikiwemo sare za Shule na madaftari.
Pia kuwepo na sheria ndogogo katika Vijiji na Kata Wilaya nzima ili mtoto yoyote ambaye hataripoti shule basi yeye na mzazi wake waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani na pia viongozi wote wa vijiji na Kata washirikiane na polisi Kata kuhakikisha kuwa wanawafatilia watoto wote ambao bado hawajaripoti katika Shule zao ambazo wamepangiwa.
Pia Mheshimiwa Mlinga ametoa wito kwa walimu wakuu wote wa shule za msingi na sekondari kuhakikisha wanawapokea wanafunzi wote hata ambao hawana sare za shule na vifaa vingine na kupunguza michango ambayo isiyo kuwa ya lazima kwasababu hii pia inachangia wanafunzi kutokuripoti kwa wakati katika shule walizo pangiwa na pia wengine kushindwa kabisa kuja shule na kukimbia.
Aidha katika kikao hicho wadau mbalimbali wamebainisha kuwa kwa Wilaya ya Liwale changamoto kubwa imekuwa kwa wazazi wamekuwa hawatoi ushirikiano na wengine pia wanawaficha watoto na kuwatorosha hivyo li lazima Serikali ihakikishe kuwa wazazi ambao hawatawajibika basi wachukuliwe hatua za kisheria kutokana na kuto wajibika ikiwemo kupelekwa mahakamani.
Kwa upande mwengine Katibu Tawala wa Wilaya ya Liwale Bi Azilongwa Mwinyimvua Bohari amewataka viongozi wote pamoja na wadau wote ikiwemo Viongozi wa Chama, Viongozi wa Dini, Watendaji wa Kata, na Vijiji kuhakikisha wanasimamia na kuyatekeleza yale yote ambayo yameazimiwa katika kikao hichi ili watoto weweze kuripoti mashule kwa sababu mpaka sasa uripoti wa wanafunzi hauridhishi.
Pia Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ndugu Winfridi Tamba amesama kuwa ni jukumu la watendaji wote wa Halmashauri ikiwemo maafisa elimu na walimu na viongozi wa Vijiji na Kata kuwa na mikakati na kuhakikisha watoto wote wanaripoti shuleni na pia amewaomba wazazi kuhakikisha wanalima mazao mengine ukiachana na yale ya mazoe hivyo walime mazao ya chakula ili kuhakikisha wazazi wanakuwa na uwezo wa kuchangia chakula cha shule ili kusaidia watoto kuripoti shule.
Hata hivyo viongozi wa dini wamehiakikishia kutoa ushirikiano kwa Serikali ikiwa kutoa elimu kupitia kwenye nyumba za ibada ili wazazi wawapeleke watoto wao mashuleni na pia wameomba walimu kuwapa majina ya watoto ambao awajaripoti shule mpaka sasa ili waweze kuwafatilia huko manyumbani kwao kwa ukaribu zaidi.
baadhi ya walimu wakuu kutoka shule mbalimbali wakiwa katika kikao cha kutathimini uripoti wa watoto mashuleni kikao hicho kimeongonza na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga
kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Ndugu Winfrid Tamba akiwapa maelekezo watendaji mbalimbali.
Polisi Kata Wa Wilaya ya Liwale wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodlauck Mlinga.
viongozi wa dini wakisikiliza maoni ya wachangiaji mbalimbali juu ya uripoti wa wanafunzi mashuleni katika Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.