Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imefanya vizuri kwa asilimia mia (100%)katika miradi yake nane iliyopitiwa na mwenge wa uhuru na kupongezwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Ismail Ally Ussi.
Akizungumza katika Uzinduzi wa nyumba za walimu 2 kwa 1 katika shule ya sekondari Kichonda Tarehe 30/05/2025 Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2025 Ndg. Ismail Ally Ussi amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mwaka huu imefanya vizuri tena kwa asilimia 100.
''Nasema hayo kwa sababu miradi yote ambayo tumeipitia na Mwenge wa Uhuru imezingatia viwango, mahitaji na sifa ya kuupa heshima Mwenge wetu wa Uhuru, ndiyo maana Mwenge huu wa Uhuru unapitishwa katika maeneo yote'' aliongeza Ndg. Ussi
Aidha Ndg. Ismail Ally Ussi amesema kuwa baada ya kukagua nyumba hizo wamejiridhisha kwa sababu nyumba zimezingatia sifa na zina mahitaji yote ambayo mtu anastahili kupata.
Mwenge wa Uhuru ulipokelewa Mei 30, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe. Goodluck Mlinga kata ya Nangano katika Kijiji cha Nangano Wilayani Liwale na kukimbizwa kwa umbali wa kilometa 117.5 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, aidha Mwenge wa Uhuru ulizindua, kuona na kuweka Mawe na Msingi katika miradi nane.
Miradi iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ni Mradi wa Maji uliopo kata ya Nangano katika kijiji cha Nangano uliogharimu Jumla ya Kiasi cha shilingi 461,448,579.00 ikiwa fedha zilizotolewa na serikali kuu ni 455,448.579.00 na Wananchi wamechangia kiasi cha 6,000,000.00 na Mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu 2 kwa moja katika shule ya Sekondari Kichonda iliyopo Kata ya Kichonda katika kijiji cha Kichonda,mradi umegharimu jumla ya kiasi cha shilingi 95,973,684.00 ikiwa fedha kiasi cha Shilingi 95,000,000.00 kimetolewa na Wahisani na Wananchi wamechangia kiasi cha Shilingi 973,684.00 na pia Mradi wa ununuzi wa gari la taka ya uliogharimu kiasi cha shilingi 239,161,161.00 ikiwa ni Fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale.
Miradi iliyopitiwa na kuonwa na Mwenge wa Uhuru 2025 ni Mradi wa upandaji miti uliopo kata ya Nangano katika Kijiji cha Nangano uliogharimu Jumla ya kiasi cha shilingi 395,000.00 Ikiwa ni fedha kutoka kwa Wahisani.Mradi wa Shamba bora la Mikorosho la Bwana Mussa. Mkoyage lililogharimu Jumla ya kiasi cha Shilingi 54,000,000.00 ikiwa ni chanzo cha fedha za Mwananchi ,
Mwenge wa Uhuru 2025 ulipitia na kuona pia mradi wa Matumizi ya Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drone) kudhibiti Changamoto za wanyama pori wakali na waharibifu uliooneshwa kata ya liwale B katika Kijiji cha Legezamwendo,mradi umegharimu jumla ya kiasi cha shilingi 81,000,000.00 ikiwa kiasi hiki kimechangiwa na serikali kuu kiasi cha Shilingi 19,000,000 na Wahisani wamechangia kiasi cha shilingi 62,000,000.00 na mradi mwingine uliopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni Mradi wa Shughuli za Vijana za Kiuchumi zilizoanzishwa kwa ufadhili wa fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri kupitia mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10 kwa Vijana,Wanawake na Walemavu,Mradi umegharimu Jumla ya kiasi cha shilingi 8,850,000.00 ikiwa Halmsahauri imetoa kiasi cha shilingi 8,000,000.00 na Wananchi kuchangia kiasi cha 850,000.00.Vijana walionufaika na mradi huu ni kutoka kata ya Likongowele katika kijiji cha Hulia.
Pia Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Ujenzi wa zahanati kijiji kata ya Kichonda katika kijiji cha Mbuli,Mradi umegharimu jumla ya kiasi cha shilingi 76,790,950.00 ikiwa kiasi cha Shilingi 60,000,000.00 kimetolewa na Serikali Kuu,10,000,000.00 kimetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Liwale na 6,790,950.00 ikiwa ni Nguvu za Wananchi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.