Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kibutuka, Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, wameibuka washindi wa nafasi ya kwanza katika kipengele cha Biological Science kwenye Mashindano ya Young Scientist Tanzania yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Washindi hao, Musa Said Mwomboka (Kidato cha Nne) na Rashidi Abdala Njumbuke (Kidato cha Tatu), waliunda timu iliyoiwakilisha Kibutuka Sekondari na kuibuka kidedea kati ya washiriki 90 waliowasilisha miradi 45 kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini.
Akizungumza baada ya kutangazwa washindi, mwalimu wao, Juma Likana, alisema ushindi huo si tu heshima kwa Kibutuka Sekondari bali pia ni hamasa kwa wanafunzi wengine kuamini uwezo wao katika ubunifu na sayansi licha ya changamoto za mazingira.
Ushindi huo unatarajiwa kuleta manufaa kadhaa ikiwemo kuitangaza shule kimkoa, kitaifa na kimataifa, kuonesha jitihada za walimu na wanafunzi katika taaluma na uvumbuzi, pamoja na kuisaidia jamii kutunza afya ya ngozi kwa kutumia bidhaa asilia badala ya vipodozi vya viwandani.
Aidha, ushindi huo umewajengea wanafunzi hao ujasiri na kujiamini kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa, na hivyo kuongeza hamasa ya kujifunza zaidi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.