Médecins Sans Frontières - Doctors without Borders (MSF) wamezindua rasmi mradi wa miaka mitatu (3) wilaya ya liwale.
Uzinduzi huo ulifanyika katika baraza maalumu liliohudhuriwa na madiwani wote wa kata, mwenyekiti wa halmashauri mh. Mohammed mtesa na viti maalumu. Wakuu wa idara, wafanyakazi na viongozi wa MSF mgeni rasmi mkuu wa wilaya Mh. Judith Nguli.
Mratibu wa mradi MSF bwana jomah kollie alielezea historia fupi ya shirika la MSF, lilianzishwa mwaka 1967 nchini nigeria.Mwaka 1993 MSF ilianzshwa rasmi nchini Tanzania lengo kuu la MSF ni kuboresha huduma za afya hasa mama na mtoto. Huduma nyingine ni kutibu magonjwa ya mlipuko, malaria, kutibu magonjwa ya afya ya akili, upasuaji, kutoa huduma katika vituo mbalimbali vya afya.
Bwana jomah kollie ameeleza kanuni na taratibu mbalimbali zinazowaongoza katika utoaji wa huduma;Kutobagua wagonjwa, kutunza siri za wagonjwa, kufanya kazi kwa uwazi, kutopokea rushwa.
Mratibu wa MSF amesema kabla ya kuja wilaya ya liwale walifanya uchunguzi wa kina katika mkoa wa lindi na kuona liwale ina mahitaji makubwa na ni wilaya iliojitenga kijiografia, iko mbali na wialaya zingine hivyo waliona kunauhitaji wakuleta mradi katika wilaya ya liwale.
MSF inashirikiana kwa ukaribu na wizara ya afya, viongozi wa wilaya na jamii kuhakikisha inatoa huduma bora.MSF imeajiri wataalamu wa afya 41 ili kuboresha huduma ya afya wilaya liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.