Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amefunga mafunzo ya ujasiriamali ambayo yameendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la WAUVI (Wanawake na Uchumi wa Viwanda ) lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa wakutengeneza bidhaa mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi.
Katika mafunzo hayo wanawake wa Wilaya ya Liwale wamepata nafasi ya kujifunza kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa Sabuni ya Maji, Batiki, Chili sosi , Jamu, Sabuni ya kipande pamoja na jinsi ya kutumia njia nzuri za kufungasha bidhaa zao ili ziweze kuingia sokoni.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka wanawake wa Liwale kuacha kufanya biashara kwa mazoea kwa sababu dunia ya sasa imebadilika hivyo ni wakati wakwenda na wakati hivyo mafunzo haya yatawasaidia kuboresha bidhaa zao ziwe na ubora ili waweze kukua kiuchumi na kukuza maendeleo ya Liwale.
Pia Mkuu wa Wilaya amewasihii kuhakikisha wanatumia vizuri mitandao ya kijamii ili kutangaza biashara zao ili waweze kuwafikia wateja mbalimbali nje na Wilaya ya Liwale na pia ametoa wito kwa Halmashauri kuendelea kutoa mikopo kwa asilimia kumi kwa kina mama ili iweze kuwakwamua na kukuza mitaji na biashara zao.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale amewataka Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Lindi kutoa ujuzi kwa vikundi mbalimbali ndani ya Wilaya ya Liwale ili viweze kutengeneza pedi ambazo ni za kushona na ambazo zitapunguza gharama na pia zitawasaidaia wafunzi mashuleni na zitapunguza utoro kwa wanafunzi wa kike.
Pia kwa upande wa changamoto Mkuu wa Wilaya mheshimiwa Mlinga amesema kuwa atahakikisha anaongea na Shirika la viwango Tanzania (Tbs) ili kusaidia na kuhakikisha bidhaa zinazo toka Liwale hususa zinazo zalishwa na vikundi vya wanawake zinakaguliwa na kuwa na ubora pindi zinapo ingia sokoni ili ziweze kuleta tija.
Aidha nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Liwale Azilongwa Mwinyimvua Bohari amewataka wanawake kuwa wamoja na kushikamana na kupena maarifa ili kujikwamua kiuchumi katika mafunzo haya ya ujasiriamali na pia kuhakikisha wanapinga ukatili wa kijinsia katika jamii kwani kwa sasa vitendo vingi vya ukatili vimeshamiri na pia kuhakikisha wanawake wanakuwa wasimamizi wazuri wa masuala ya elimu kwa mtoto wa kike kwani mtoto wakike akipata elimu itakuwa imemkomboa napia kuachana na mila ambazo hazileti ustawi katika jamii .
baadhi ya matukio ambayo Mkuu Wa Wilaya mheshimiwa Goodlauck Mlinga ameyaona wakati wa ufungaji wa mafunzo ya wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali .
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.