MKUU WA WILAYA ASHIRIKI BARAZA LA MADIWANI
Mkuu wa wilaya ya Liwale Mh. Judith Nguli amewapongeza wakuu wa idara kwa kufanya kazi vizuri na kujituma, amewaasa kuwa makini katika kila hatua ya kazi wanazozifanya, usimamizi wa miradi na kutunza kumbukumbu vizuri.Vile Vile amewashukuru waheshimiwa madiwani na kamati zote kwa kazi mbalimbali, na ushirikiano wao wa bega kwa bega pia amewasisitiza kua anashukuru michango yao kwenye maswala mbalimbali kwasababu inasaidia kujitathmini na kufanya kazi zetu kwa ufanisi zaidi ili kuendana na kasi ya Mh. Rais
Amemshukuru Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa nyingi za miradi ya maendeleo kwenye halmashauri ya Wilaya ya Liwale na amewaomba wakuu wa idara kusimamia miradi hii kwa uadilifu, sambamba na hilo, amempongeza mkaguzi wa ndani ndugu Alphonce Akarrow kwa kufanya kazi vizuri na kuonyesha madhaifu mbalimbali kwaajili ya kurekebisha.
Mkuu wa wilaya Liwale Mh. Judith Nguli pia amewapongeza waheshimiwa madiwani kufwatilia kwa ukaribu swala la madini, amewaomba wakuu wa idara husika kuendelea kutathimini na kufanya utafiti ni namna gani madini yatatuongezea mapato. Kamati ya ulinzi na usalama inazunguka kwenye migodi yote kuhakikisha wenye vitalu wamekata leseni, pia kuhakiki hali ya usalama kwa kupeleka askari kwenye migodi ili kuimarisha ulinzi wa wachimbaji na wananchi kwa ujumla.
Mh. Mkuu wa wilaya amesema kwenye swala la mifugo kamati ya ulinzi na usalama imefanya doria kwenye maeneo yote yenye changamoto ya ng'ombe na wamekamata baadhi ya wafugaji ambao wapo kinyume na sheria.Tayari rasimu ya sheria ndogo ya udhibiti na usimamizi wa mifugo imeshaandaliwa na amewashukuru waheshimiwa Madiwani kuipitisha, hivyo imebaki hatua chache kuanza kutumia sheria hiyo na hatimaye ufumbuzi wa tatizo la ng'ombe litapatikana. Aidha Mh. Judith Nguli ameahidi kuwa atatembelea maeneo yote ya wafugaji na kuongea na wafugaji wote. Ameomba waheshimiwa Madiwani kutoa ushirikiano na kutoa taarifa ya aina yoyote ya usaliti na rushwa kwenye swala hili la mifugo.Pia amezungumzia juu ya ujenzi wa kituo cha askari wa wanyama pori ambapo ameeleza kuwa kimejengwa na kimekamilika na tunarajia askari wa wanyama pori kuongezwa ili kuongeza hali ya usalama dhidi ya wanyama pori hususani Tembo.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.