Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mheshimiwa Goodluck Mlinga, akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Wilaya, Bi. Azilongwa Bohari, pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, ametembelea Kitalu cha Uwindaji wa Kitalii cha Hokororo kilichopo chini ya mwekezaji Wembere Hunting Safaris katika eneo la Hifadhi ya Wanyamapori ya Magingo.
Ziara hiyo iliyofanyika Alhamisi, Novemba 20, 2025, ililenga kukagua shughuli za uhifadhi, kujionea hali ya wanyamapori, na kudumisha uhusiano kati ya Serikali na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Magingo.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya alipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za uwindaji wa kitalii pamoja na mafanikio yaliyopatikana. Aidha, alizungumza na uongozi wa Jumuiya hiyo kuhusu namna bora ya kuboresha usimamizi wa rasilimali za wanyamapori ili kuendelea kunufaisha wananchi wa vijiji vinavyoizunguka hifadhi.
Mheshimiwa Mlinga alisisitiza umuhimu wa kuimarisha usalama, kudhibiti uharibifu wa mazingira na kuongeza ushirikiano kati ya Serikali, wadau wa uhifadhi na wananchi. Viongozi wa Magingo WMA waliishukuru Serikali kwa ufuatiliaji huo na kuahidi kuendelea kuimarisha uhifadhi na kuendeleza uhusiano mzuri wenye manufaa kwa jamii.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.