• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Liwale District Council
Liwale District Council

Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Uhasibu
      • Miundo Mbinu
      • Afya
      • Usafishaji na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Mifugo
    • Vivutio vya kitalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Ugani
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Mipango na Fedha
      • Uchumi na Mazingira
      • Community Services
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo mbalimbali
  • KItuo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi na kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mlinga atoa Pole Kijiji cha Makata

Imewekwa:: September 22nd, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga leo ametembelea kijiji cha Makata Kitongoji cha Chekanenda na kutoa pole kwa familia pamoja na jamii baada ya mkazi wa kijiji hicho bwana Mohamed Shomari Kapuja umri wa miaka 45 kuuwawa na tembo.

Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa tatatizo ni kubwa na bado Serikali inazidi kupambana na tatizo hilo hili kuondoa changamoto iyo aidha pia amewakumbusha ahadi ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya kuchukua changamoto iyo na kwenda kuifanyia kazi katika ngazi ya kitaifa ili kuondoa changamoto iyo ya wanyama waharibufu tembo ambao wamekuwa wakileta madhara kwa jamii.

Aidha Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mlinga amesema jitihada zinazo chukuliwa na Wilaya ni kubwa kuhakikisha wanapambana na wanyama hao pia amewapongeza Taasisi ya wanyama pori TAWA kwajinsi wanavyo pambana na tembo kuhakikisha wanawatoa mbali na makazi ya watu lakini bado tatizo nikubwa ndani ya wilaya hii.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kuna mradi wa ambao umeisha tambulishwa na utatambulishwa hivi karibuni katika vijiji vyote ambao ni kati ya Serikali ya Tanzania pamoja na Serikali ya Ujerumani kwajili ya kupambana na tembo pamoja na wanyama haribifu na lengo la mradi huo ni kutoa mafunzo kwa wananchi pamoja na makundi na kutoa pia vitendeakazi kwajili ya kupambana na tembo.

Pia Mkuu wa Wilaya amewahakikishia wananchi wa kijiji cha Makata kuwa ataendelea kuwatumia askari wa wanyama pori pamoja na kusimamia miradi ambayo italetwa ili kuhakikisha wanakabiliana na tembo ambao ni waharibifu katika mazingira yetu na hata hivyo kwa tembo ambao wamekuwa wakiwauwa watu Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa ataendelea kutafuta kibali ili kuwaondoa wasiendelee kuleta madhara kwa watu.

Nae mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mohamed Mutesa ametoa  pole kwa wananchi wa kijiji cha  makata na kuwataka kuwa wastahimilivu kipindi hiki kigumu huku jitihada zikiendelea kuchukuliwa na serikali yao pia amwewataka wananchi kuhakikisha wanaacha kihifadhi mabibo ndani kwa msimu huu wa korosho tembo wamekuwa ni wengi  wakifuta mabibo hivyo wanavyo sikia harufu ya mabibo basi wanakuja na pia  amewataka kuchukua tahadhari pindi wanapokuwa wapo kwenye mashamba yao kwa msimu huu wa korosho.

Nae msimamizi wa Taasisi ya Wanyama pori TAWA Wilaya ya Liwale ndugu Chacha amewakumbusha wananchi wa vijiji vyote kuhakikisha wanachukua taadhari katika kipindi hichi na pia kutoa taarifa kwani kwa sasa kumekuwa na makundi ya tembo yanazunguka sehemu mbalimbali hivyo  pindi wanapo yaona watoe taarifa kwa wakati kabla madhara ayajotokea.

 

Ndugu Chacha kutoka Taasisi ya wanyama pori TAWA akiwaelezea wananchi wa Kijiji cha Makata jinsi ya kuchukua taadhiri pindi tembo wanapokuwa wamevamia maeneo yao.

Mkuu wa wilaya ya Liwale Mhesimiwa Goodluck Mlinga pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri wakiwasikiliza Wananchi wa Kijiji cha Makata baada ya kifo cha mtu mmoja kilichosababishwa na tembo.

Wananchi wa kijiji cha Makata wakiwasikiliza wataalamu wa wanyama pori .

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO AWAMU YA PILI KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 February 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MKATABA MSF May 07, 2025
  • TANGAZO LA KUANZA KWA MFUMO MPYA WA TAUSI KWA AJILI YA UTOAJI HUDUMA YA MALIPO MBALIMBALI YA SERIKALI KWA NJIA YA MTANDAO February 20, 2023
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI October 09, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • HISTORIA IMEANDIKWA, HALMASHAURI YA WILAYA YA LIWALE YAFANYA VIZURI KWA 100% KATIKA MIRADI ILIYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 30, 2025
  • WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI (BVR KIT) JIMBO LA LIWALE WAPATIWA MAFUNZO

    May 14, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LIWALE YAPOKEA TUZO YA GLASS YA ELIMU KIMKOA KWA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA KWA MWAKA 2024

    May 02, 2025
  • UFUNGWAJI YA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA.

    November 01, 2024
  • Angalia Zote

Video

Video nyingine

Viunganishi vya Haraka

  • www.tamisemi.go.tz
  • Kupata Hati ya Mshahara (Salary Slip) kwa Watumishi wa Umma
  • Bodi ya Ajira
  • Utabiri wa Hali ya Hewa
  • Taarifa za huduma ya elimu
  • Taarifa za huduma ya afya

Tovuti Linganifu

  • Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Linndi RS
  • Ruangwa
  • Nachingwea
  • Lindi Manispaa

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Dissertation-Writingservice.com

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters

    Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE

    Simu ya Mezani: 023 2937043

    Mawasiliano ya mkononi:

    Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz

Anuani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.