Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Zainab Telack, ameonesha kukerwa naucheleweshaji wa ujenzi wa daraja lililopo Kijiji na Kata ya Kimambi katikaHalmashauri ya Wilaya ya Liwale, linalotekelezwa na Kampuni ya Ukandarasi ya Mbuya.
Mheshimiwa Telack alionyesha kutoridhishwa nakasi ya ujenzi huo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi yaujenzi wa madaraja makubwa wilayani Liwale, akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzina Usalama ya Mkoa wa Lindi pamoja na Kamati ya Ulinzina Usalama ya Wilaya ya Liwale.
Amesema ucheleweshaji wa mradi huo ni jambolisilokubalika, hasa ikizingatiwa kuwa mkandarasi huyo tayari amepokea fedha zamradi kwa hati ya dharura na kuandikiwa zaidi ya barua 12 za maonyo bilakuchukua hatua za kuridhisha.
“Mkandarasi huyu amepewa fedha na muda wakutosha kukamilisha kazi kabla ya mvua kuanza, lakini hadi sasa hakunamaendeleo yanayoonekana. Naagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ukandarasiya Mbuya kufika ofisini kwangu ifikapo Oktoba 22, 2025, kueleza sababu zaucheleweshaji huu,” alisema Mheshimiwa Telack.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa alitembelea miradimingine ya ujenzi wa madaraja katika Kata za Kibutuka na Nangano,ambako aliwataka wakandarasi husika kuongeza kasi ya utekelezaji wa kazi ilimiradi hiyo ikamilike kwa wakati.
Ameagizawakandarasi wote kufanya kazi usiku na mchana, kuongeza wafanyakazi na vifaa,ili kuhakikisha madaraja hayo yanakamilika kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua,akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia uzembe au ucheleweshaji wa miradi yamaendeleo yenye manufaa kwa wananchi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.