Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainab Telack amewapongeza wafanyakazi kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kujenga Taifa na kuleta maendeleo katika eneo lake la kazi na kuendelea kutumikia wananchi ameyasema hayo katika sherehe za wafanya kazi Meimosi ambazo zimefanyika Kimkoa katika Wilaya ya Ruangwa.
Mheshimiwa Telack amewataka wafanyakazi kuhakikisha wanatumia vizuri muda wao wakazi ili kuleta maendeleo katika sehemu husika kumekuwa na baadhi ya wafanyakazi wanatumia muda wa muajiri katika mambo yao binafsi jambo ambalo sio zuri na linazorotesha maendeleo hivyo kila mtumishi ahakikishe anatumia muda vizuri katika eneo la kazi na kucha kutumia simu na kuchati.
Hata hivyo Mheshimiwa Telack amewataka waajiri kuhakikisha wanashirikiana na wafanyakazi na kuwasikiliza na kutatua kero zao kwani kumekuwa na watumishi wengi wanamalalamiko hivyo wanawajibu wakuwasikiliza na kuwalipa stahiki zao na kutatua kero zao ili waweze kufanya kazi kwa bidii na kuleta maendelo katika Mkoa wetu.
Aidha Mheshimiwa Telack amewataka watumishi wote waserikali kuhakikisha wanakuwa na maadili mazuri na lugha za staha katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuwahudumia watanzania mbalimbali na pia itasaidia kujenga ushirikiano na ambao utatusaidia kuleta maendeleo hivyo tuwe watiifu kwa tunao wahudumia katika maeneo yetu.
pia Mheshimiwa Telack amewataka watumishi kupinga vitendo vya rushwa na vitendo vya unyanyasaji katika maeneo ya kazi kwani hii inachangia kudhohofisha molari za watumishi na kufanya watumishi kutokuwajibika hivyo niwaombe watumishi tuwe waadilifu na kukemea vitendo hivi ili tuweze kufanya kazi kwa usawa na kuwapa wananchi maendeleo.
Hata hivyo Mheshimiwa Telack amewataka waajiri kuhakikisha wanawapa watumishi nafasi za kujiendeleza kimasomo kama sheria inavyo sema hii itasaidia kuzalisha watumishi wenye uwezo mkubwa wa kusaidia serikali katika mipango yake na watumishi tuhakikishe tunatumia nafasi hizi kwa uwadilifu kwani kumekuwa na watumishi ambao wanakimbia kujiendeleza sababu ya kuaribu katika nafasi zao za kazi hivyo tuwe wasafi na waadilifu.
Mheshimiwa Telack amewaagiza waajiri wote katika Mkoa wa Lindi kuhakikisha wanalinda maslahi ya watumishi na kuyasimamia na pia kuandaa mafao ya watumishi wanao staafu katika vituo vyao vya kazi na pia watumishi wahakikishe wanatimiza majukumu yao ipasvyo serikali imesikia changamoto zote ambazo zimewasilishwa na zitafashiwa kazi hivyo tushirikiane na serikali ili tuweze kujenga taifa na kuleta maendeleo katika Mkoa wetu.
Picha mbalimbali katika matukio ya sherehe za meimosi zilizofanyika Wilaya ya Ruangwa.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.