Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Sport Development Aid wamezindua na kukabidhi vifaa vya michezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Ndugu Tina Sekambo ikiwa ni muendelezo wa kusapoti Sekta ya Michezo mashuleni kwa Shule za Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ambapo shule 16 za sekondari zimekaidhiwa vifaa hivyo.
Mkurugenzi wa Mradi wa Sport Development Aid Ramson Lucas amesema mradi ambao wanaendelea nao kwa Shule za Sekondari ujulikanao kama Empowering Boys’ Society Through Sport and Health Education ni mradi ambao unalengo la kumsaidia kijana wa kiume katika kutambua nafasi yake katika jamii sambamba na kupinga mfumo dume na pia kumjengea uwezo wa kujitambua.
Aidha Ramson ametoa rai kwa wadau wengine kuhakikisha wanaweka mkazo katika suala la physical education kuwa sehemu ya masomo mengine kwa kuhakikisha kupitia michezo na mazingira ya shule yanakuwa rafiki kwa kujifunzia kwa sababubu michezo ni chanzo cha ajira.
Kwa upande mwengine Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Ndugu Tina sekambo amewashukuru wadau hawa muhimu katika kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za kukuza na kuendeleza michezo katika mashule jambo litakalosaidia kuwalinda vijana na kuwaunganisha na kuwajengea tabia njema hata hivyo amewaomba waangalie jinsi ya kuwasaidia pia wanafunzi wa elimu ya msingi kwa kuwapatia vifaa vya michezo ili nao waweze kujihusisha na michezo kwa sababu michezo ni afya.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri amewataka Maafisa Elimu kuhakikisha wanatenga muda wa michezo katika shule zote ili wanafunzi waweze kushiriki vizuri michezo kwa sababu michezo ni ajira na itasaidia kuwatengenezea uwezo wa kujitambua na kuwaepusha na tabia zisizofaa katika jamii.
Picha malimbali katika uzinduzi na kukabizi vifaa vya michezo vilivyo tolewa na Sport Development Aid.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.