VIJIJI 27 VYA WILAYA YA LIWALE KUNUFAIKA NA PROGRAMU/MRADI WA KUENDELEZA MNYORORO WA THAMANI YA MAZAO YA MISITU.
Wilaya ya Liwale ni moja kati ya Wilaya Tatu (3) za Mkoa wa Lindi ambazo zitanufaika na “PROGRAMU YA KUENDELEZA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO YA MISITU” kupitia ufadhili wa serikali ya Finland kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Program hii imezinduliwa tarehe 19/06/2019 katika ukumbi wa halmsahauri na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Mohamed Mtesa. Aidha wakati wa uzinduzi Mwenyekiti wa Halmashauri aliwaasa waheshimiwa madiwani kuukubali mradi, kuusimamia na kuwahamasisha wananchi kuzingatia maelezo ya program ili kufikia matokeo tarajiwa.
Wakati huo huo nae Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mh. Sarah Chiwamba alisisitizaa juu ya Muundo wa Utekelezaji wa Program hii Kitaifa na Kuukaribisha Mradi huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale.
Semina hii ya utambulisho wa programu ya kuendeleza mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu iliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ilishirikisha wajumbe wakiwemo Mh. Mkuu wa Wilaya, Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri, Mh. Mkurgenzi wa Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Halmashauri huku wakiongozwa na Mwezeshaji wa Semina Ndg. Eustace Boniface.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.