Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainab Telack amefanya kikao na wafugaji wa Wilaya ya Liwale akiwaeleza lengo la Serikali lakuwagawia maeneo ya kuchungia ili kuondoa na kudhibiti mifugo inayodhurula na kulishwa kwenye mashamba ya watu jambao linalao sababisha migogogro na upotevu wa amani kati ya wakulima na wafugaji.
Mheshimiwa Telack amesema kuwa jambo kubwa ni kutafuta suluhu na kuelewana ili kuepusha migogoro hii na kuwataka wafugaji wote kujisajili na kupata idadi kamili ya wafugaji na mifugo yao ili wanapo pewa maeneo hayo yaendane na idadi ya mifugo hata hivyo Mkoa wa Lindi umetenga maeneo mbalimbali kwa ajili ya ufugaji “niwatake wafugaji mtoe idadi kamili ya mifugo yenu ili mpatiwe maeneo ambayo yataendana na mifugo yenu na tusitoe taarifa za uwongo Serikali hipo kwa ajili ya kuwasaidia nyie na sio kuwanyanganya mifugo yenu kama vile watu wengine wanavyo wadanganya”.
Hata hivyo Mheshimiwa Telack amewataka wafugaji wote ambao watapewa maeneo ya kufugia ambayo yanendelea kupimwa sehemu mbalimbali ndani ya Mkoa wa Lindi ikiwemo hapa Liwale” wanawajibu wa kuyaendeleza kwa kuchimba visima na kupanda nyasi kwaajili ya mifugo yao na mfugaji ambaye hatafanya hivyo ajue kuwa ndani ya Mkoa huu ata hama na pia hatutaki wafugaji ambao wanadhurula hovyo na mifugo kwenye mapori na hifadhi za Serikali na kulisha kwenye mashamba ya watu”.
Aidha Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Telack amekiagiza Chama Cha Wafugaji Tanzania kiendelee kutoa elimu kwa wafugaji kwani wengi wao wamekuwa na uwelewa mdogo juu ya kugawiwa maeneo ya kufugia hivyo tushirikiane na Serikali ili tuweze kutatua changamoto hii ambayo ipo ndani ya Mkoa huu tunaitaji kufuga kisasa tuache kumiliki ngombe wengi ambao awana tija tukifuga kisasa tupata faida nyingi.
Mheshimiwa Telack amewambia wafugaji kuwa kufuga kisasa kutasaidia kukaa na mifugo eneo moja na kucha kudhurula tumeona Serikali inatafuta masoko ya nyama nnje ya nnchi kufuga kisasa itasaidia kupata soko la uwakika kwasabubu mifugo yenu itakuwa ikakauguliwa marakwa mara na maafisa mifugo wetu ambao wapo na pia Serikali itajua kuni dadi ngapi ya mifugo ambayo ipo ndani ya Mkoa ili iweze kutoa chanjo kwa wafugaji wote ambao wapo.
Aidha Mweshimiwa Telack amewataka wafugaji kuwa na utaratibu wa kuvuna na kupunguza idadi ya mifugo yao kwani kuwa na idadi kubwa ya mifugo imekuwa inawanyima haki watoto wa jamii ya kifugaji kupata elimu badala yake wanakuwa wanadhurula na mifugo kwenye mapori hivyo wafugaji mnatakiwa kubadilika na pia itawasaidia kutambulika na pia kudhaminiwa na Taasisi za kifedha ikiwemo mabenki ambayo yatawapatia mikopo mfuge kisasa ili tutoke huku tulipo.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Zainab Telack amekiataka Chama Cha wafugaji Tanzania kuhakikisha kinasimamia na kupata uongozi mpya wa wafugaji wa Liwale ambao watashirikiana na Serikali katika zoezi hili la kuwagawia maneo na kuwa mstari wa mbele kuwasidia wafugaji na kuwapa elimu ili tuweze kuanza maisha mapya kati ya wafugaji na wakulima katika Mkoa huu na pia wananchi wote wa Lindi wanataka amani hivyo wafugaji tutimize haya ambayo tumekubaliana.
Picha mbalimbali ikiwemo Kamati ya Usalama ya Mkoa na Wilaya pamoja watumishi na wafugaji wakisikiliza maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainab Telack katika kikao cha wafugaji Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.