Zaidi ya wagonjwa 360 wamejitokeza na kupata huduma za kibingwa katika Hospitali ya Wilaya ya Liwale, kufuatia ujio wa jopo la madaktari bingwa waliotoa huduma mbalimbali kuanzia tarehe 15 hadi 19 Septemba 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya hospitali hiyo, wagonjwa 158 walihudumiwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani, 39 na Daktari Bingwa wa Watoto, 41 na Daktari Bingwa wa Upasuaji, 88 na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akina Mama, na 37 na Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno.
Aidha, jumla ya upasuaji mdogo 5 na mkubwa 5 ulifanyika kwa ushirikiano wa Daktari Bingwa wa Usingizi na Ganzi na madaktari wa upasuaji.
Huduma hizo ni sehemu ya jitihada za Serikali kusogeza matibabu maalum karibu na wananchi, kwa lengo la kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za afya na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora kwa gharama nafuu karibu na makazi yake.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.