Katibu Tawala Mkoa Ndugu Ngusa Samike akiongozana na Mganga Mkuu Mkoa bwana Herry Karia, Bi Albina Gelege meneja mradi USAID Afya na bwana Ezekiel Buliana Famasia wa Mkoa. amefanya Ziara Katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kwa Lengo la Kukagua Huduma za Afya Zinazotolewa, Upande wa Famasia, Mama na Mtoto na huduma Inayotolewa kwa Waathirika wa Virusi vya Ukimwi(VVU)
Pia Kuhakiki Utekelezaji wa Maagizo ya Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa alipohutubia Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Asilimia 50 ya Mapato Yanayokusanywa Kwenye Vituo vya Afya Zitumike Kununulia Madawa, Vifaa Tiba na Lishe. Ambapo alifanya ziara kwenye vituo vifuatavyo.
Alikagua hali ya ujenzi wa mradi na kupongeza wahandisi kusimamia vizuri, aliwataka Halmashauri kutoa pesa iliobaki na kumaliza majengo yaliyobaki na hospitali ianze kufanya kazi.
Katibu tawala Mkoa alikagua Hosptali ya wilaya Liwale upande wa kliniki ambapo alisifu kuwepo kwa rejesta ya dalili za hatari na kusisitiza umuhimu wa kuweka taarifa za kutosha za wagonjwa ili kupunguza hatari kwa mama na mtoto, amekagua ugaaji neti, amekagua hali ya ugawaji wa dawa ya fefo na kukagua vifaa vya kutolea huduma.
Amekagua upande wa pharmacy amepongeza watumishi kuboresha huduma ya kutoa dawa ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Kituo cha Afya Mpengele amekagua jengo la RCH, amekagua chanjo za Watoto. Mganga Mkuu Mkoa amewasihi watumishi kufanya usimamizi wa karibu wa chanjo hizo ili kuleta ufanisi wa ugawaji wa chanjo hizo.
Katibu tawala Mkoa amekagua nyumba za watumishi ambao ni mradi wa Uviko ambao ulikamilika tarehe 30/07/2022, aliwapongeza wahandisi kusimamia vizuri mradi huo
Mganga mkuu Mkoa aliwataka viongozi wa kituo hiko kuongeza idadi yaa vipimo ili kuendana na hadhi ya kituo cha afya.
Kituo cha afya Mpengele wanakabiliwa na changamoto za upungufu wa watumishi, na changamoto ya vifaa kama Kompyuta.
Katibu tawala Mkoa alikagua upande wa RCH, alikagua hali ya ugawaji wa dawa ya fefo, folic acid, daftari la dalili za hatari na alikagua hali ya utoaji huduma, Bi Albina Gelege meneja mradi USAID Afya,liwapongea kutoa huduma nzuri.
Pia alikagua upande wa CTC alikagua huduma ya utoaji wa dawa kwa waathirika wa vvu, hali ya upimaji wa VVU na upimaji w avira load, Katibu tawala Mkoa aliridhishwa na huduma inayotolewa pia Mganga mkuu mkoa Herry Karia alisistiza kuhamasisha watu kujitokeza kupima vvu hasa wanaume.
Amekagua upande wa pharmacy amepongeza haliya huduma kuboreshwa ukilinganishwa na kipindi cha nyuma.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.