Mkuu wa Wilaya Liwale amefanya Ziara kwenye Kijiji cha Naluleo kata ya Liwale Mjini, aliwashukuru wananchi kushiriki vyema katika zoezi la sensa, wananchi walipata fursa ya kutaja changamoto zao ambazo ni:
Changamoto ya Wanyama pori: Mh. Mkuu wa wilaya alitoa ufafanuzi juu ya changamoto hiyo kua askari wa Wanyama Pori wameongezwa na kituo kikubwa askari wa Wanyama pori kinajengwa Kijiji cha NGUMBU
Afisa Tawala ndugu Alexander Malela aliomba wananchi kusajili mapema ili wapate vyeti vya kuzaliwa ilikuepuka changamoto ya kukosa huduma kwa sababu ya kukosa vyeti hivyo.
Afisa uhamiaji Mrakibu Kemilembe Balongo aliwaasa wananchi kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji pale watakapo kua na mashaka na mtu yeyotekatika kipind hiki cha msimu wa korosho kwasababu wilaya ya Liwale inapokea wageni kutoka sehemu mbalimbali.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.