ZIARA YA WAHESHIMIWA MAWAZIRI, MH. MASHIMBA NDAKI WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI NA MH. HAMADI MASAUNI WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA LIWALE.
Ziara hiyo ni agizo la Mh. Raisi Mama Samia Suluh Hassan kutembelea maeneo yenye changamoto za wafugaji na wakulima na changamoto za wanyama pori. Waheshimiwa mawaziri wamefanya ziara hiyo katika kijiji cha Lineng'ene kata ya Mirui na kijiji cha Kibutuka kata Kibutuka. Maeneo hayo yote yanakabiliwa na changamoto za wafugaji na wanyama pori, wananchi wameeleza namna wafugaji wanavyo wasumbua, wafugaji wanaharibu mazao ya wakulima na kuwajeruhi, wamekua tishio kwao kiasi cha kuathiri hali kiuchumi kwenye vijiji hivyo, changamoto ya kupata mazao kidogo kwasababu ng'ombe wanaingia kwenye mashamba ya wakulima. Pia Wananchi wamelalamikia changamoto ya wanyama pori hususani Tembo. Wanyama hawa wanaingia mpaka kwenye makazi ya wananchi, tembo wanafanya uharibifu wa mazao na inasabisha kupata hasara ya mazao na kupata chakula kidogo au kukosa kabisa. Tembo wanahatariaha maisha ya wananchi na baadhi ya wananchi wamepoteza maisha kwa kujeruhiwa na tembo.
Waheshimiwa mawaziri wametoa utatuzi wa changamoto hizi kwa kutoa maelekezo kuhakikisha hawa wafugaji wote wamehamishwa kutoka maeneo yote yasiyo rasmi na kupelekwa maeneo rasmi kwaajili ya wafugaji. Wananchi wameombwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye operesheni hii rasmi ili kukomesha changamoto hii. Viongozi wa vijiji kufanya wajibu wao na kuhakikisha wananchi wanapata haki zao. Waheshimiwa mawaziri wameomba kila mtu afanye wajibu wake kwanzia mwananchi, uongozi wa kijiji mpaka ngaz ya wilaya. Kwa sasa maaskari wa kata wamewekwa kila kata kusimamia ulinzi na usalama wa wananchi hivyo tuwatumie askari hawa pindi changamoto itakapotokea, mawasiliano ya askari kata zimetolewa kwa wananchi kurahisisha mawasiliano ili kuimarisha usalama. Sambamba na hili ng'ombe wakirudi kwenye maeneo rasmi changamoto ya tembo itapungua, Waheshimiwa mawaziri wamesema changamoto zingine zitaendelea kupewa utatuzi na wataendelea kutoa maelekezo ili kumaliza changamoto hizi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.