TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za Kazi za Mteknolojia Dawa Msaidizi kama ifuatavyo;
1. MTEKNOLOJIA DAWA MSAIDIZI – NAFASI TATU (3)
A. KAZI NA MAJUKUMU YA MTEKNOLOJIA DAWA MSAIDIZI.
i. Kuainisha, kuandaa na kuagiza mahitaji ya dawa na vifaa tiba katika eneo lake la kazi.
ii. Kuuza dawa na vifaa tiba kwa wateja/wagonjwa.
iii. Kuhifadhi dawa na vifaa tiba.
iv. Kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa.
v. Kukagua dawa, vifaa tiba kemikali, vitendanishi na vipodozi katika Duka la Dawa la Hospitali.
vi. Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa.
vii. Kushiriki kazi za kamati ya usimamizi wa Duka la Dawa la Hospitali.
viii. Kuandaa taarifa ya matumizi ya dawa na vifaa tiba.
ix. Kufanya uchunguzi wa ubora wa dawa, vifaa tiba kemikali, vitendanishi na vipodozi.
x. Kufanya kaguzi mbalimbali katika sehemu zinazohifadhi dawa.
xi. Kusimamia utendaji wa kazi watumishi walio chini yake.
xii. Kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba pamoja na taarifa za mwezi za Duka la Dawa.
xiii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
B. SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe na Astashahada/Cheti (Certificate) katika fani ya Uteknolojia dawa wasaidizi kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wafamasia.
C. MSHAHARA
Kwa kuzingatia waraka wa Serikali mshahara ni TGHS A.
MASHARTI YA KAZI/WAOMBAJI KWA UJUMLA
i. Awe raia wa Tanzania.
ii. Awe na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45
iii. Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
iv. Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIN).
v. Nafasi ya Kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua.
vi. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (a detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika pamoja na namba zao za simu.
vii. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma na mafunzo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali:
- Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV
- Cheti cha mafunzo (professional).
- Cheti cha kuzaliwa.
- Picha Moja “Passport Size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
- Usajili kamili (Full Registration) au Leseni hai ya kufanya kazi ya taaluma husika.
viii. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali.
ix. Waombaji walioajiriwa kwa mkataba wa ajira kutoka kwa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Afya wanatakiwa kuambatisha nakala za mkataba na barua za uthibitisho kutoka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri husika.
x. Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma.
xi. “Testimonials”, “Provisional results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form IV and form Vi result slips) HAVITAKUBALIWA.
xii. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi zitapelekea wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
xiii. Nakala za vyeti vyote viwe vimethibitishwa (Certified copies).
xiv. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 16/03/2023 saa 9:30 alasiri.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kwa njia ya posta kwa anuani ifuatayo.
Barua zote zitumwe kwa anwani iliyopo hapa chini.
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA,
S.L.P 23,
LIWALE.
Aidha, barua za maombi zinaweza kuwasilishwa moja kwa moja katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale.
Limetolewa na;
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA,
LIWALE
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.