Wilaya ya Liwale ilianzishwa rasmi Julai 7, 1975 baada ya kumegwa kutoka Nachingwea kutokana na ukubwa wa Wilaya ya Nachingwea. Kabla ya hapo, Wilaya ya Liwale ilikuwa ni Tarafa ya Wilaya ya Nachingwea toka mwaka 1961. Pia katika mwaka 1975, Wilaya ikawa Jimbo rasmi la Uchaguzi ambapo Mbunge wa kwanza alikuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu Marehemu Rashid Mfaume Kawawa.
Baada ya kumegwa kutoka Nachingwea, Wilaya ya Liwale imekuwa ni miongoni mwa Halmashauri sitazinazounda mkoa wa Lindi; hii ni pamoja na Halmashauri za Wilaya za Kilwa, Lindi, Ruangwa, Nachingwea na Lindi Manispaa.
Wilaya ya Liwale ilikuwa Halmashauri ilipofika Mwaka 1984. Hapo ikawa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambayo ilikuwa na madaraka kamili kama yalivyoainishwa katika Sheria ya uanzishaji wa Mamlaka hizo ya Mwaka 1982.
Kijiografia Liwale inapatikana kati ya Latitudo 80na 10050`Kusini mwa mstari wa Ikweta na pia Longitudo 36050`na 38048`Mashariki.
Wilaya ya Liwale imepakana na Wilaya za Nachingwea upande wa kusini, Wilaya ya Ruangwa upande wa kusini mashariki, Wilaya ya Kilwa upande wa mashariki; Wilaya ya Rufiji upande wa kaskazini, Wilaya ya Mahenge upande wa kaskazini-magharibi na Wilaya ya Tunduru upande wa kusini-magharibi.
Liwale ina eneo la kilometaza mraba 38,380 ambalo ni zaidi ya nusu ya eneo lote la Mkoa waLindi. Kati ya eneo hilo zaidi ya 2/3 ni misitu yenye kilometa za mraba 27,965.4. Mgawanyo wake ni kama ifuatavyo; Hifadhi ya Mbuga ya Selous kilometa za mraba 25,587,(Hii ni 2/3 ya eneo lote la Wilaya). Hifadhi ya Msitu wa Angaikilometa za mraba 1,394.20 na Hifadhi ya Msitu wa Serikali Kuu wa Nyera–Kipelele wenye kilometa za mraba 984.20. Eneo lililosalialenye kilometa za mraba 12,793 ambazo ni sawa na theluthi moja ya eneo lote la Wilaya linatumika kwa makazi, mipaka “buffer zone,”kilimo na shughuli nyingine za uchumi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.