MAJUKUMU YA IDARA YA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII
Kuraghabishi jamii ili iweze kujiletea maendeleo yao endelevu kwa kutumia rasilimali walizonazo wenyewe.
Kufanya tafiti ndogondogo shirikishi za kijamii na kiuchumi ili kubaini matatizo waliyonayo na kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo kwa kutumia mpango wa fursa na vikwazo.
Kuihamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi ili kumpunguzia mwanamke mzigo wa kazi
Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali kutoka sekta zote katika Halmashauri ya wilaya ambayo inahitaji ushirikishaji jamii
Kusajili na kuzisimamia asasi zisizo za kiserikali kutokana na ukweli kuwa asasi hizi ni washirika wa Halmashauri na Serikali kwa ujumla katika mchakato wa maendeleo.
Kukusanya Takwimu za kijamii, kutunza, kutafsiri na kusambaza Takwimu hizo kwa matumizi ya jamii kwa kuzingatia shughuli za sekta nyingine.
Kupambana na umaskini wa kipato kwa kuratibu utoaji na urejeshaji wa mikopo kwa wanawake na vijana kutokana na mifuko mbalimbali kama vile Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake(WDF) na Mfuko wa vijana.
Kuendeleza na kukidhi mahitaji ya makundi maalum katika jamii ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa dawati la jinsia kwa kila Idara.
Kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
Kuelimisha na kuihamasisha jamii juu ya mila potofu zote zinazoweza kukwamisha jitihada za Wananchi katika kujiletea maendeleo yao kama vile mauaji ya vikongwe, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino) na ukeketaji wa wanawake (Female Genital Mutilation)
Huduma kwa makundi maalum watu wenye ulemavu, watoto waishio katika mazingira hatarishi na wazee
Huduma kwa familia, watoto na vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.
Huduma za majaribio na ujenzi wa tabia (Probation)
Kuratibu na kuboresha mitaala ya kufundishia stadi mbalimbali za maisha kwa vijana katika NGOs CBOs na Vituo vya Vijana.
Kuratibu shughuli za Maendeleo ya Vijana katika Vituo ,NGOs na CBOs Wilayani
Kupanga, kusimamia na kuendesha mafunzo ya ujasiri kwa vijana ili kuwawezesha kukabiliana na matatizo yanayojitokeza katika maisha
Kuratibu shughuli za usajili wa NGOs na CBOs zinazofanywa na Wilaya
Kuhamasisha na kushauri juu ya uanzishaji wa vituo vya vijana katika wilaya na kuratibu na kusimamia mfuko wa Vijana (YDF)
Kukusanya taarifa mbalimbali muhimu,Kutafsiri na kusambaza kwa jamii
Kuratibu mafunzo ya utoaji wa mbinu za kuwasaidia vijana kujikomboa na umasikini, ujinga na kupiga vita UKIMWI ,madawa ya kulevya na kutetea usawa wa jinsia.
Kufanya uchambuzi wa matatizo ya jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Halmashauri,
Kuhamasisha uandaaji wa mipango ya uwiano ya Maendeleo ya Wilaya
Kuvisaidia vikundi maalum (ushirika/CBOs/kidini) kuandaa Miradi (project write –up)na kuwawezesha namna ya kupata miradi.
Kusimamia utekelezaji wa Sera za maendeleo za fani mbalimbali katika wilaya
Kuwaongoza na kuwasimamia, watumishi wa Maendeleo ya jamii wa ngazi ya Tarafa, kata na vijiji
Kuratibu na kusimamia mafunzo ya viongozi wa vijiji na vikundi mbali mbali vya maendeleo wilayani.
Kukusanya taarifa mbalimbali muhimu na kusisambaza kwa jamii
Kuandaa mikutano ya maafisa maendeleo ya jamii wa kata kuzungumzia matatizo,mafanikio na kuandaa mikakati ya uboreshaji wa Maisha/ Maendeleo ya wananchi katika Tarafa
Kueneza elimu ya uraia mwema na kuratibu kazi za Uraghibishi katika Idara na Taasisi zingine
Kuandaa, kuhakiki na kupendekeza maombi ya mikopo ya vikundi na kupokea marejesho ya mikopo
Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu,wazee, malezi ya watoto na familia zenye matatizo
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji vituo vya kulelea watoto mchana, malezi yakambo, na vyuo vya walezi wa watoto wadogo mchana
Kupokea,kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akinamama waliojifungua watoto watatu au zaidi kwa wakati mmoja
Kupokea, kuchambua nakuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali.
Kupokea, kuchambua nakuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki
Kuhoji na kuandaa taarifa za washtakiwa
Kusimamia wahudumiwa katika makazi, vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi vya watu wenye ulemavu, mahabusu za watoto na shule za maadilisho
Kuihamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi ili kumpunguzia mwanamke mzigo wa kazi
Kusimamia ujenzi wa nyumba bora vijijini
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.