MAJUKUMU YA IDARA YA MIFUGO NA MAENDELEO YA UVUVI
Kutafsiri sera za mifugo, uvuvi, mikakati, miongozo na kanuni kulingana na hali ya mifugo na uvuvi kiwilaya;
Kuhakikisha maandalizi ya mipango ya maendeleo ya mifugo kulingana na mahitaji ya wafugaji katika njia shirikishi;
Kuwezesha kuunganisha utafiti na huduma za ugani na kutengeneza mahusiano mazuri kwa kuwashirikisha wakulima, vikundi vya wakulima, viongozi wa wilaya, viongozi wa vijiji na kata na maafisa wa halmashauri;
Kutengeneza miongozo ya watoa huduma binafsi (CBO’s, NGO’s) na watoa huduma binafsi wakubwa na kuwawezesha waweze kufanya mikataba na halmashauri katika kutoa huduma katika halmashauri.
Kuweza kusimamia utoaji wa zabuni haraka na kutoa maamuzi haraka na kwa wakati kwa kuzingatia vigezo na masharti.
Kuweka miongozo ya matumizi ya tafifiti zinazoonesha matokeo mazuri kwa makundi husika (wafugaji na wavuvi) katika halmashauri.
Kuweka ushirikiano kati ya taasisi na mawakala wanaofanya kazi za mtambuka na halmashauri ya wilaya kama: maliasili, jinsia, mazingira, wakala wa uwezeshaji wa mkoa (RFAs) katika kumbambana na virusi vya ukimwi na ukimwi ili kuhakikisha kuwa masuala haya yanazingatiwa katika mipango kazi kuwezesha ufugaji na uvuvi endelevu.
Kuunganisha na kusimamia kazi zote za mifugo na uvuvi zinazofanywa katika Halmashauri na watoa huduma wa jamii na binafsi. Kufuatilia, kusunganisha na kutoa taarifa ya magonjwa na wadudu waenezao magonjwa wanaohamahama katika ngazi zinazohusika na udhibiti katika kanda, mikoa na taifa.
Kuandaa taarifa za utekelezaji za mwezi, robo mwaka na mwaka za maendeleo ya mifugo na uvuvi na kuhakikisha zinawasilishwa kwa mkurugenzi mtendaji, mkoa, kanda na wizarani.
Kuandaa na kuwasilisha taarifa ya mwaka ya utendaji kazi wa watumishi wa idara ya mifugo na uvuvi.
Kutathmini mahitaji ya pembejeo za mifugo na uvuvi, upatikaji na usambazaji katika halmashauri ya wilaya.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.