Mkuu wa wilaya ya liwale mhe Goodluck Mlinga amefunga rasmi mafunzo ya jeshi la akiba leo tarehe 01 Novemba, 2024 katika viwanja vya shule ya msingi kibutuka kata ya kibutuka. Mafunzo hayo yalianza rasmi 04 julai 2024 ambayo yamechukua takribani miezi mine kukamilika, jumla ya wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo ni wanawake 05, wanaume 33 na kufanya jumla ya 38.
Askari hao wamepewa mafunzo mbalimbali ikiwemo mbinu za kivita, ujanja wa porini,silaha ndogo, usalama wa taifa, usalama wa ndani, huduma ya kwanza, kuzuia na kupambana na rushwa na uraia.
Mafunzo hayo yamewafanya askari hao kuawafanya kua majasiri na wakakamavu hivyo wako tayari kushiriki katika maswala ya ulinzi wa taifa bila woga wowote. Pia askari hao wamejifunza shughuli mbalimbali za kijamii kama kuchangia damu.
Aidha mhe. Mkuu wa wilaya ameipongeza halmashauri ya wilaya ya liwale kuchangia sare za askari hao kiasi cha shilingi milioni sita . pia amewashukuru wananchi wa kibutuka kua sehemu ya kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi.
Pia amemuagiza makamu mwenyekiti wa halmashauri mhe. Mohammed likoko, halmashauri kuweka mkakati rasmi wa kuwatumia jeshi la akiba katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kitaifa. Pia amesisitiza kuwa askari wa jeshi la akiba ni askarikamili na
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.