KAZI ZA IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI
|
· Kuandaa na kuwasilisha kwenye Mamlaka husika Ikama na Bajeti ya Watumishi wa Halmashauri (PE) pamoja na Bajeti ya Matumizi Mengineyo ya Idara
|
|
|
|
· Kuandaa malipo mbalimbali ya watumishi na watoa huduma kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya fedha.
|
|
· Kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi wa Halmashauri
|
|
|
|
· Kutafsiri Sheria, Kanuni, Taratibu, na Miongozo mbalimbali ya Utumishi wa Umma
|
|
· Kuandaa/kuhuisha TANGE na kuiwasilisha kwenye mamlaka husika
|
|
· Kushughulikia vibali vya ajira, mikataba, upandishwaji vyeo na kuthibitisha watumishi kazini.
|
|
· Kuandaa na kuwasilisha taarifa mbalimbali za utekelezaji za utumishi kama TUU
|
|
· Kuratibu zoezi la Upimaji wa Utendaji kazi wa Wazi (OPRAS) wa watumishi wote na kutoa taarifa baada ya mwaka kuisha
|
|
|
|
· Kuratibu na kusimamia shughuli za usafiri na usafishaji kwenye Idara na masuala ya utawala.
|
|
· Kushughulikia stahili mbalimbali za watumishi (likizo, matibabu, mazishi, mafao, ruhusa na usafiri).
|
|
· Kuratibu utekelezaji wa vikao vya kisheria ngazi ya Makao Makuu, Kata, Vijiji na Vitongoji
|
|
· Kushughulikia uingizaji na marekebisho mbalimbali ya watumishi kwenye Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS).
|
|
· Kuratibu shughuli za Uchaguzi ngazi ya Vijiji na Vitongoji na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
|
|
· Kusimamia nyumba za Halmashauri ngazi ya Makao Makuu, Kata na vijiji.
|
|
· Kuratibu kero mbalimbali zinazojitokeza na kushughulikia na kutoa taarifa ya utekelezaji kila robo mwaka.
|
|
· Kusimamia mafunzo ya watumishi ya muda mfupi na mrefu kulingana na mahitaji ya mafunzo na mpango wa mafunzo
|
|
|
|
· Kuratibu ziara za viongozi mbalimbali wanaofika Wilayani
|
|
· Kusimamia matumizi salama ya nyaraka za Serikali na vifaa vya Ofisi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
|
|
· Kuagiza vifaa na huduma mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi kwa mujibu wa bajeti.
|
|
· Kuratibu sherehe na matamasha mbalimbali ya Kitaifa, Kimkoa na Wilaya kwa mujibu wa ratiba
|
|
· Kusimamia mawasiliano ya kiofisi kwa ngazi zote za kiutendaji ndani ya Wilaya na nje ya Wilaya.
|
|
· Katibu wa vikao vya Bodi ya Ajira, Menejimenti, Kamati ya Maadili ya Madiwani na Kamati ya Uadilifu ya Watumishi.
|
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.