MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU MSINGI
Kupanga, kuratibu na kusimamia masuala yote ya Idara ya Elimu katika Wilaya
Kupanua na kuimarisha Elimu ya Msingi na kusimamia wajibu na maslahi ya watumishi katika Idara ya Elimu
Kukagua na kufuatilia taarifa za ukaguzi wa Elimu ya Msingi
Kuandaa na kusimamia uendeshaji wa mitihani ya Elimu ya Msingi hasa darasa la IV na VII ya Taifa kila mwaka.
Kusimamia mgawo na mipango ya fedha kwa ajili ya uendeshaji masuala ya kielimu
Kuwaendeleza walimu kitaaluma ili watoe huduma bora zinazokidhi viwango
Kufuatilia ufundishaji katika shule za msingi na kusimamia mtaala wa elimu
Kukusanya takwimu za watahiniwa wa darasa la IV na VII kutoka shuleni kuzihakiki na kuziwasilisha Mkoani kila mwaka
Kufuatilia taarifa ya ukaguzi wa Elimu ya Msingi, kufuatilia na kutoa ushauri kwa walimu juu ya utekelezaji wa mitaala ya elimu
Kufuatilia ufundishaji katika shuel za msingi na kusimamia mtaala wa elimu
Kufuatilia taarifa ya ukaguzi wa Elimu ya Msingi, ufuatilia na kutoa ushauri kwa walimu juu ya utekelezaji wa mitaala ya elimu
Kuagiza na kusambaza vifaa vya elimu katika shule, kugawa fedha na kusimamia matumizi ya fedha katika shule
Kubaini na kusimamia ikama ya walimu katika shule, kusimamia na kufuatilia miradi ya ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, vyoo na utengenezaji samani za shule
Kusimamia na kufuatilia fedha zinazotolewa kwa ajili ya kuendesha Elimu ya Watu Wazima
Kuratibu utoaji wa Elimu ya Sekondari katika vituo vya ufundi stadi na watu binafsi nje ya mfmo rasmi.
Kusimamia uanzishaji na uendeshaji wa maktaba za Kata na Vijiji
Kushirikiana na sekta za Afya, M/jamii na mashirika ya Umma kuendeleza Elimu Maalum kwa shule za Msingi na Sekondari
Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya utoaji wa elimu katika shule, Kutunza kumbukumbu za vifaa vya kufundishia na kujifunzia
Kupanga, kuratibu na kusimamia michezo, kusimamia sera za michezo na utamaduni wa Kitanzania katika shule za msingi
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.