MAJUKUMU YA KITENGO CHA MALIASILI NA MAZINGIRA
Kusimamia Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 na kutekeleza Sera ya Wanyamapori, kufanya doria katika maeneo yenye wanyamapori na kutunza nyara za serikali kabla ya kuziwasilisha katika ghala la Taifa
Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii kwenye wilaya husika na kukusanya maduhuli ya serikali kwa kutoa leseni za uwindaji wa wenyeji (local hunting) kwenye maeneo ya wazi kulingana na quota iliyotolewa
Kusimamia uwindaji wa wenyeji na wageni wakaazi na kutunza kumbukumbu na takwimu za wanyamapori, kukusanya taarifa zinazohusu aina, idadi na mienendo ya wanyamapori na kuwasilisha idara ya wanyamapori kwa utaratibu, tathmini pamoja na mambo mengine na kupanga quota.
Kulinda wananchi na mali zao dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu na kutoa mafunzo kwa jamii juu ya uhifadhi wa wanyamapori
Kuwa kiungo kati ya wananchi na Idara ya Wanyamapori katika shughuli za ushirikishwaji wa wananchi katika uhifadhi
Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu uhifadhi wa wanyamapori hasa kwa wananchi waliotenga maeneo ya uhifadhi katika ardhi yao, kulingana na sheria, sera na miongozo itakayotolewa na Idara ya Wanyamapori
Kuandaa mipango ya maendeleo kuhusiana na wanyamapori
Kusimamia matumizi endelevu ya misitu ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
Kukusanya maduhuli ya serikali kwa kutoa leseni za matumizi ya misitu
Kusimamia Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 na kutekeleza Sera ya taifa ya Misitu
Kutoa elimu ya sheria ya Ardhi Na. 4 na 5 ya mwaka 1999
Kutoa elimu juu ya sera ya ardhi na maendeleo ya makazi na suala zima la upangaji na usimamizi wa miji
Kuandaa na kutoa Hati miliki za ardhi na kupima mashamba na viwanja vya makazi
Kuandaa na kuwezesha mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji, kutafsiri na kupima mipaka ya maeneo ya utawala
Kufungua masjala za vijiji za ardhi na kuandaa na kukabidhi vyeti vya vijiji
Kusambaza sheria za ardhi, kuandaa mipango ya jumla na mipango ya kina ya mipangomiji na kusimamia ukuaji wa miji
Kufanya uthamini wa ardhi na mali za kudumu na kutatua migogoro ya ardhi na kuchora ramani
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.