Mhe. Goodluck mlinga, mkuu wa Wilaya ya Liwale akitoa salamu katika mkutano wa kawaida wa baraza la halmashauri leo tarehe 30 Oktoba 2024 lililofanyika katika hospitali ya wilaya ya Liwale.
Mhe. Mlinga amempongeza Mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Mohammed Mtesa na waheshimiwa madiwani wote kwa kufanya kazi kwa umoja na kutunza maelewano kati yao, pia amewapongeza wakuu wa idara kwa kufanya kazi kwa ushirikiano, kushirikisha changamoto zozote kwake. Amewapongeza timu ya halmashauri kwa kufanya kazi nzuri kwenye zoezi la kujiandikisha na kupata matokeo ya 91.8% ya uandikishaji. Amewaasa madiwiani kua mabalozi wa kuhamasisha amani katika maeneo yao katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, amewaahidi yeye na kamati yake nzima ya ulinzi na usalama kuhakikisha Amani itakuepo muda wote.
Mhe. Mlinga ametoa rai kwa idara ya ujenzi na miundombinu na manunuzi kuhakikisha miradi yote ya sekondari ya kata ya Lilombe, Mpigamiti na kuchochorokana ikamilike na ianze kutumika ifikapo januari 2025.
Pia amemshukuru mhe. Rais Dkt Samia Suluh Hassan kwa kuleta umeme katika vijiji vyote vya Wilaya ya Liwale ikiwemo kijiji cha Ndapata ambacho kipo mbioni kuwashwa umeme.
Aidha mhe. Mlinga amewataka waheshimiwa madiwani kusimamia swala zima la utoro kwa wanafunzi na kutokomeza changamoto ya utoro mashuleni. Pia amewataka madiwani kusisitiza halmashauri za vijiji kuchangia chakula kwenye taasisi za shule ili kutokomeza swala la utoro mashuleni. Aidha Mwenyekiti wa Halmashuari Mhe. Mohammed Mtesa amewataka waheshimiwa madiwani kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika siku ya tarehe 27. Novemba, 2024 ili kuchagua viongozi watakao wasimamia katika maeneo yao. Pia amewataka waheshimiwa madiwani kuhamasisha wananchi kutumia pesa za kororsho kwa mambo yenye manufaa ikiwemo ujenzi wa nyumba bora na kuwekeza katika elimu.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.