Kata ya Mlembwe
Diwani wa kata ya Mlembwe aliwasilisha taarifa ya utekelezaji katika Kata ya Mlembwe kipindi cha robo ya kwanza (Julai- Septemba, 2017). Katika Kata hiyo Baraza lilipokea:- Taarifa ya idadi ya watu,Taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo, Maendeleo ya kilimo, Maendeleo ya Elimu ya Msingi na Sekondari, Dhana ya uzalendo na hali ya utawala bora,mafanikio na changamoto zilizojitokeza.
Katika kujadili taarifa hiyo ilitolewa hoja ya tatizo la mganga katika Zahanati ya Ndapata na walishaahidiwa kupatiwa mtumishi huyo.
Maelezo yalitolewa kuwa Mganga Mkuu Mkoa amekumbushwa hoja hiyo.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. Box 23 Liwale
Simu ya Mezani: +255 (0) 737 187 605
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2018 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.