Waandikishaji wasaidizi wa daftari la kudumu la mpiga kura na Waendesha vifaa vya Bayometriki Jimbo la Liwale Leo Mei 14, 2025 wamepatiwa mafunzo kwa ajili uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura awamu wa pili.
Akizungumza baada ya kufungua mafunzo hayo Afisa Mwandikishaji Jimbo la Liwale Ndg. Winfried Tamba Amewataka waandikishaji kuzingatia makundi maalumu ya watu ikiwemo wazee na wajawazito ili wawe wa kwanza kupatiwa huduma pia kuzingata mavazi yenye heshima na lugha mzuri wanapokuwa katika kazi.
Aidha Ndg. Tamba amewataka waandikishaji hao kutunza vifaa vitakavyotumika katika uandikishaji ili viweze kudumu kwa muda mrefu zaidi.
Kwa upande wake Afisa Tehama kutoka Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Ndg. Sylivester Kisigo amewataka waandikishaji kutoa hamasa kwa wananchi ambao mwanzo hawakupata nafasi ya kujiandikisha waje wajiandikishe kwani zoezi hilo litafanyika ndani ya wiki moja tu.
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya pili litaanza rasmi tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 22 Mei 2025.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.