Thursday 30th, January 2025
@
UTT (Unit Trust of Tanzania) AMIS inawajengea uwezo wa kiuchumi watumishi.
Watumishi wa almashauri ya wilaya ya liwale wametakiwa kujijengea uwezo wakuweka akiba ili kujiwezesha kukua kiuchumi na kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha mafunzo ayo yametolewa na taasisi ya UTT AMIS iliyo chini ya serikali na wizara ya fedha na mipamgo.
Katika mafunzo hayo watumishi wameelezwa kuwa lengo la ni kuwawezesha wananchi kujiwekea akiba na kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji kulingana na makubaliano yaliyo ainishwa kwenye waraka wa toleo wa mfuko husika.
Pia katika mafunzo hayo watumishi walifahamishwa juu ya faida za kuwekeza katika mfuko huu ikiwemo ufanisi wa kiitaalamu katika kuendesha mfuko huo , urahisi wa muwekezaji anaweza kufatilia maendeleo ya masoko ya fedha, unafuu kwa muwekezaji kutumia gharama nafuu katika uwekezaji, faida inatoa nzuri ukilinganisha na bidhaa za aina iyo , ukwasi urahisi wa kujiunga na kujitoa na faida nyinginezo .
Aidha, watumishi walishauriwa kuchagua aina za mifuko kutoka UTT ikiwemo hati fungani , watoto fund , ukwasi fund, mfuko wa kujikimu ambayo itawasaidia kukuza kipato chao na pia kutatua baadhi ya changamoto zinazo wakabili na pia kupunguza matumizi yasiyo kuwa na lazima kufanya ivyo itawasaidia kukuwa kiuchumi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.