Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amehidi kuchangia mifuko 50 ya saruji kwajili ya ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha makinda ametoa ahadi hiyo katika mkutano wa hadhara katika ziara Kata ya Mangirikiti.
Mheshimiwa Mlinga amefanya ziara ya Kata ya Mangirikiti kwenye vijiji vya Makinda, Kipule, na Mkonganage ikiwa ni kusikiliza Kero za wananchi na kuzitolea majibu Mheshimiwa Mlinga amewataka wananchi wa Kijiji cha Makinda kuanza kukusanya nguvu kutoka kwa wananchi na tozo za makato ya mazao ili kuanzisha boma na baadae Serikali italeta fedha ili Kijiji kiweze kupata zahanati na kuhudumia watu.
Akijibu kero za wananchi wa Makinda Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa kero ya wanyama haribifu tembo ni kubwa kwa Wilaya ya Liwale hivyo jitihada zinafanyika katika kuhakikisha tunawatoa tembo hawa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani imeleta mradi wa GIZ ambapo vijan 132 watachukuliwa kutoka ndani ya Wilaya yetu na kupewa mafunzo na vifaa jinsi ya kupambana wanyama hao.
Pia Serikali imeendelea na mikakati ya kitaifa kuhakikisha kuwa wanyama haribifu Kama hawa tembo wanaweza kudhibitiwa na wasilete madhara kwa binadamu na hata kuharibu mazao na kuhatarisha usalama wa watu ndio maana Serikali imejenga vituo ikiwemo ngumbu na pia Askari wa wanyamapori Tawa na a fisa wanyamapori wamekuwa wakipambana ili wasilete madhara.
Aidha Mheshimiwa Mlinga amesema kuhusu wafugaji Halmashauri imepitisha Sheria ambayo inadhibiti mifugo hivyo wafugaji wote ambao wapo maeneo ambayo siyo ya wafugaji waondoke Mara moja na pia amezitaka Serikali za vijiji kuhakikisha zina kuwa na jukumu la kulinda raia na usalama wa vijiji kwani vijiji vyetu vina kamati za ulinzi hivyo tuzitumie katika kujilinda na mifugo. Hata hivyo amewaonya baadhi ya viongozi wa vijiji kuchukua rushwa kutoka kwa wafugaji kwani vitendo hivyo vinachangia maeneo yetu kuharibiwa na mifugo hivyo tuwe wadilifu.
Katika kero nyingine ikiwemo miondombinu ya elimu Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa Serikali bado inaendelea kutoa fedha kwajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo elimu hivyo kwa madarasa amabayo ni chakavu, na ujenzi wa nyumba za walimu utakuja kwa awamu na pia amezitaka Serikali za vijiji kutumia mapato ya ndani kwa kuanza miradi Kama hii na Serikali kuu itaweka nguvu.
Kwa upande wa umeme Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa Serikali imetoa billion 34 kwa aajili ya kusambaza umeme katika vijiji vyote vya Wilaya ya Liwale vijiji 76 hivyo vyote vitafikiwa na umeme.
Na pia kuhusu barabara na maji serikali inaendelea kufanyia kazi kwani wataalamu mbalimbali wapo kazini wakifanya tathimini na watakapo tuletea majibu basi utekelezaji utaanza maara moja
Hivyo kikubwa nikuendele kutoa ushirikiano kwa Serikali na yote ambayo yamesemwa basi yatafanyiwa kazi kwa haraka ili wananchi wetu wapate maendeleo kama kusudi la Serikali.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mangirikiti wakifatilia na kusikiliza majibu ya kero zao wakati Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Goodluck Mlinga akijibu.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.