Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amekagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kichonda ambapo jumla ya shilingi milioni 560,5552, 827 zimepokelewa ili kukamilisha ujenzi huo ambao utapunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda kusoma Kata jirani.
Ujenzi huo ni pamoja na jengo lenye vyumba 2, jengo lenye vyumba vya madarasa 2 na ofisi 1, jengo la Utawala 1, jengo la maabara ya kemia na baolojia 1, jengo la maabara ya fizikia 1, maktaba 1, chumba cha TEHAMA 1, jengo la vyoo vya wavulana na wasichana 1, matundu 4 yakiwa na huduma kwa wenye mahitaji maalumu, jengo la vyoo vya wanafunzi wasichana matundu 4 yakiwa na huduma kwa wenye mahitaji maalumu, kichomea taka, na tanki la maji la ardhini.
Mheshimiwa Mlinga amesema” nimeridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule ya Kichonda na pia nawapongeza wananchi wa Kata ya kichonda kwa kuendelea kujitolea ili kuhakikisha ujenzi huu unakamilika kwa wakati kama ilivyo pangwa kuwa mwisho wa mwezi wa kumi mradi uwe umekamilika”.
Aidha mheshimiwa Mlinga ametoa rai kwa wasimamizi wa mradi huo kuwa nilazima ukamilike kwa wakati na kuhakikisha ubora wa majengo unazingatiwa na pia watu wote wanao fanya kazi katika mradi huu basi walipwe haki zao kwa wakati ikiwemo mafundi pamoja na vibarua wote.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga akipokea ripoti ya ujenzi wa shule ya Sekondari Kichonda
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.