Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wametembelea vyanzo vya maji vya Wilaya lengo likiwa ni kukagua na kuangalia uwezo wakutoa maji na kuwahudumia wananchi wa maeneo husika na utunzaji wa vyanzo hivyo.
Mheshimiwa Mlinga ametembelea chanzo cha maji Barakiwa ambacho kina hudumia vijijiji vitatu vya Barikiwa, Chimbuko, na Ndunyungu na inakadiriwa kuwa na watumiaji 5,320. Mheshimiwa Mlinga amewataka wakazi wa Barikiwa kuhakikisha wanatunza vyazo vya maji kwa kuacha kulima na kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji kuendelea kuwepo kwa shughuli hizo zitasababisha kupoteza vyazo vya maji na hata kukauka na wananchi kukosa huduma ya maji.
Pia Mheshimiwa Mlinga ametembelea chanzo cha maji Ngongowele ambacho kipo katika msitu wa Hangai ambacho kitahudumia vijiji vya Ngongowele , Mikuyu, ,Darajani na Mihimo ambapo inakadiriwa kuwa na watumiaji 12,190 pia amekagua ujenzi wa mradi huo kwenye chanzo cha maji na kukagua ujenzi wa ntaki kubwa moja na sehemu ya mfereji pamoja na mtandao wa maji kwenda kweye tanki kubwa la maji na ujenzi wa mradi huo unakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi Tshs 958,975,215.00 kukamilika kwa maradi huo.
Aidha Mheshimiwa Mlinga ametembelea chanzo cha maji cha Turuki amabacho kinategemewa kusambaza maji eneo la Liwale mjini na maeneo ya Makonjiganga, Muungurumo, Likongowele, Mpirani, Ulia, Nganyaga, Kuchochorokana, Kilipwike, Lindota, Kinguluwila, Liwale B, Naluleo, Mbonde, Nangando na Turuki na watumiaji wanakadiriwa kuwa 34,382 pia amewataka Wakala wa Maji Vijijini Ruwasa eneo la Liwale Kuhakikisha wanalinda chanzo hicho kwani kinategemewa na idadi kubwa ya watu hivyo ameshauri kuhakikisha kuwa kinalindwa dhidi ya mifugo na wanao kata miti hovyo na wanao lima kando kando ya vyanzo vya maji.
Sambamba na kutembelea vyanzo hivyo Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Goodluck Mlinga ametembelea chanzo cha maji cha Nangano ambacho kimekamilika na kinatoa huduma kwa wananchi wa maeneoa hayo na watumiaji wanakadiriwa kuwa 1,880 ambao wanapata maji safi na salama na pia amewewataka wananchi kutumia maji ya bomba ambayo ni safi na kuacha kutumia maji ya mto mbwemkulu ambao umekuwa ukitumiwa na wafugaji kunyweshea mifugo yao maji na pia wachimbaji wa madini kutiririsha sumu ambayo ni hatari kwa afya zao.
Pia Mheshimiwa Mlinga ametembela na kukagua chanzo cha maji na ujenzi wa mradi wa maji wa Kitogoro na Kiangara ambao unakdiriwa kuwa na watumiaji 4,535 ambao watapata maji safi na salama katika maeneo hayo yote hivyo Wakala wa maji vijijini Ruwasa wametakiwa kuongeza kasi hili kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Liwale wanapata huduma ya maji safi.
Baada ya kutembelea vyanzo hivyo vya maji katika Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Mlinga ametoa maelekezo amewataka Wakala wa Maji vijijini Ruwasa kuhakikisha wanasimamia miradi yote ambayo ipo na ikamilike kwa wakati na wananchi wapate huduma ya maji, pia kuhakikisha wanasambaza vilula vya kuchotea maji maeneo yote ambayo yana uhitaji ikiwemo Mashuleni na kwenye Vituo vya Afya na Zahanati.
Kwa upande mwingine amewataka kuhakikisha wanasimamia na kutunza vyazo vyote vya maji ikiwemo kuwaondoa wale wote ambao wanalima au wanafanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo ya vyanzo ikiwemo pembe zoni mwa mto Liwale kwa mujibu wa sheria na utaratibu.
Picha mbalimbli katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Liwale kukagua vyanzo vya maji na miradi ya maji.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.