Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amepiga marufuku kuendelea na shughuli za uchimbaji wa madini katika kijiji cha Lilombe baada ya kubaini kuwa shughuli hizo zinafanyika bila kuwa na kibali na kutofuta utaratibu na sheria hivyo kusbabisha uharibifu mkubwa wa mazingira husasa pembezoni mwa mto Mbwemkulu na mto Nguramiga eneo la Liwale.
Mheshimiwa Mlinga amefanya ziara hiyo katika kijiji cha Lilombe sambamba na eneo la mto Mbwemkulu eneo la Liwale na kujionea uharibifu mkubwa uliofanywa na wachimbaji wa madini raia wa China ambao wanafanya shughuli hizo pembezoni mwa mto Mbwemkulu ikiwemo kuhamisha mto na kufukia njia ya mto na ikumbukwe mto huo ndio mpaka mkubwa kati ya Wilaya ya Liwale na Nachingwea. Hata hivyo Mheshimiwa Mlinga amebaini kuwepo na uharibifu upande wa vyanzo vya maji katika maeneo hayo jambo linalopelekea wananchi wa vijiji jirani kukosa maji na pia kuwepo na sumu ambazo wanatumia katika kusafishia na kunasa madini ya dhahabu.
Aidha Mheshimiwa Mlinga ametembelea eneo la mto Ngurumaiga kijiji cha Lilombe na kujionea kambi mbili za raia wa China ambazo zinafanya shughuli hizo za uchimbaji wa madini zikiwa na vifaa vya kisasa ikiwemo mashine kubwa za kuchumbia , mashine kubwa za kuoshea, na pampu kubwa za kuvuta maji kwajili ya kuoshea madini hayo hata hivyo “Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa wachimbaji hawa awana leseni wala kibali na pia hakuna taarifa yeyote walio toa kwenye wilaya hivyo huu ni uvamizi katika eneo letu” na hivyo kuwtaka wafike ofisini na nyaraka zote ambazo zinawapa uhalali wa kuchimba madini katika eneo la Wilaya ya Liwale
Kwa upande mwengine Mheshimiwa Mlinga amewataka wananchi na viongozi wa vijiji jirani kuhakikisha wanatoa taarifa kwa viongozi wa wilaya pindi wanapo ona hali kama hizi zinatokea katika maeneo haya kwasababu uharibifu wa mazingira ni mkubwa sana hususa eneo la mito hivyo tunaomba mtupe ushirikiano ili tuweze kuzuia uharibifu huu na kuwachukulia sheria pia wahusika hawa wote.
Picha mbalimbali za uchimbaji wa madini katika Kijiji cha Lilombe.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.