Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amekutana na Watendaji wa Vijiji na Kata pamoja na Wenyeviti wa Kamati za Maliasili na Makatibu wake katika kikao kazi cha kupena miongozo na kusimamia mapato yatokanayo na misitu katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Liwale day.
Mheshimiwa Mlinga amewataka viongozi wote wa vijiji na Kata kuhakikisha wanasimamia nakutimiza majukumu yao katika ngazi za vijiji na Kata kwani wengi wao wamekuwa wakifanya mambo ambayo yasiyo mazuri viongozi wamekuwa ndio chanzo cha migogoro na kupoteza mapato kwa kuwapokea wafugaji bila kufuata utaratibu , wamekuwa wakiuza maeneo kiholela watumishi wengi hawashindi katika vituo vyao vya kazi badala yake wamekuwa wakizurula mjini, hivyo kushindwa kisimamia mapato ya vijiji yatokanayo na misitu, hivyo ameagiza kila mtumishi akae eneo lake la kazi ni marufuku kuja mjini.
Aidha amekumbusha kuwepo na Kamati za ulinzi na usalama katika vijiji kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi wa maeneo hayo kwani kwa sasa ni msimu wa korosho hivyo matukio ya uhalifu yanaongezaka kamati hizi zikatekeleze majukumu yake ikiwa kulinda karosho kwenye mashamba pia ameagiza viongozi wa vijiji kusimamia lishe kwakufuata miongozo ambayo wanapewa na wataalamu.
Aidha Mheshimiwa Mlinga amezitaka Kamati za Maliasili kuhakikisha zinasimamia sheria na taratibu na pia kukusanya mapato ambayo yanatokona na maliasili ya misitu hivyo amazitika kamati hizo kuacha kufoji nyaraka , kuacha kuwapa wafanyabiashara leseni bila kufuata utaratibu, napia kusimamia wafanyabiashara wavune eneo ambalo amepewa na sio kuongeza ujazo wa eneo, na pia kuacha kupitisha wavunaji wengi kuliko eneo ambalo wanalo kwani ni kosa kufanya hivyo na tutashughulika na wale wote ambao wamehusika na toa wito kwa wale wote ambao wanadaiwa walipe hakuna mvunaji ambaye ataendelea kuvuna kama anadaiwa .
Hata hivyo Mheshimiwa Mlinga amezitaka kamati kucha kushirikiana na wafanyabiashara kwani kufanya hivyo ni kuhujumu na kupoteza mapato ya Serikali bali wasimamie sheria na taratibu ambazo zipo aidha Mheshimiwa Mlinga ameagiaza viwanda vyote kucha kufanya kazi nyakati za usiku bali wafanye kazi mchana tu na hivyo wale wanao daiwa walipe na pia viongozi wote mkasimamie fedha na mapato yetu pamoja na miradi ya Serikali.
Picha mbalimbali katikia kikao kazi cha Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga na watendaji wa vijiji , kata na wenyeviti na makatibu wa maliasili.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.