Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga ametoa onyo kwa makarani wote na Vyama vya Msingi vyote mtu yoyote atakaye msababishia mkulima hasara atalipa yeye mwenyewe na nimarafuku kulipa madeni kwa kutumia fedha za ushuru wa mazao ameyasema hayo katika ziara ya kukagua maghala Liwale mjini ambayo yanatumika kukusanya ufuta kwa sasa.
Mheshimiwa Mlinga ametembelea na kukagua maghala na mizani ambazo zinatumika kupimia ufuta katika vyama vya Umoja Amcos, Likongowele Amcos, pamoja na Tumaini Amcos amewataka makarani kuhakikisha wanarekodi taarifa kamili za mkulima ili kuweza kuepusha hasara ambazo zinaweza kujitokeza katika msimu huu wa ufuta na pia kuaangalia ubora wa ufuta ambao unaletwa na wakulima na kuhakikisha hakuna ufuta ambao ni mchafu unao kusanywa.
Hata hivyo Mheshimiwa Mlinga ametoa rai kwa vyama vyote vya Msingi katika Wilaya ya Liwale Kuhakikisha vinasimamia vizuru ushuru wa mazo ambao unapatikana na kucha kutumia vibaya au kulipa madeni ambayo wamesababisha wao badala yake fedha hizo zitumike katika kuendeleza vyama vyao ili viweze kujiendesha kibiashara.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.