Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe. Goodcluk Mlinga amezindua maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani ambapo kwa Wilaya ya Liwale jumla ya chanjo 2500 zitatolewa kwa Mbwa katiaka vijiji vyote vilivyopo Wilaya ya Liwale na kutoa elimu kwa jamii juu ya Ugonjwa huu hatari unaowapata Mbwa.
Akizungumza na wataalamu na wananchi waliojitokeza katika amaadhimisho hayo ya chanjo ya kichaa cha mbwa katika viwanja vya Ujenzi Liwale Mjini, Mkuu wa Wilaya ya Liwale amewashukuru wasimamizi wa chanjo hizo na kuwataka kutoa chanjo kwa kupita kila sehemu katika wilaya nzima ili kutoa huduma hii kwa jamii japo ni ngumu lakini pia kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watoa chanjo.
Siku ya kichaa cha Mbwa Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Septemba 2023 kwa lengo la kuhamasisha jamii kutokomeza ugonjwa huu wa kichaa cha mbwa ambapo maadhimisho haya kitaifa yalizinduliwa rasmi tarehe 24 Septemba na Waziri wa mifugo Mhe. Abdallah Ulega na kufungwa na Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa tarehe 28 Septemba 2023 ndipo kilele cha maadhimisho hayo.
Sambamba na hayo katika risala ilioandaliwa na Ofisi ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kusomwa mbele ya mgeni rasmi inaeleza kuwa kampeni hiyo ya chanjo itausisha vijiji vyote vilivyopo mji wa liwale bila malipo yoyote ambapo matarajio ni kutoa chanjo 2500 kutokana na chanjo zilizopokelewa ivyo matumaini makubwa ni kuwafikia watu wote wanaofuga Mbwa na Paka waweze kupata chanjo.
Takwimu zilizopo zinzonesha kuwa kati ya Januari 2021 hadi Septemba 2023 idadi ya matukio ya watu kuumwa na Mbwa ni 42 katika kipindi cha mwaka wa 2022 pekee jumla ya matukio 19 yalioripotiwa pia Serikali inatambua vijiji vilivyo athirika ni Pamoja na Ngunja kata ya ngowele, Lilombe Kata ya Lilombe, Kinguluila Kata ya Nangando.
Hata ivyo jumla ya Mbwa na Paka 94 walichanjwa katika maeneo yaliyoathirika ikiuhusisha kata ya Lilombe, Ngongowele, Kimambi, Liwale Mjini Likongowele, na Nangando. Hata ivyo kwa kipindi cha Januari 2012 hadi Septemba 2023 hakuna vifo vilivyo ripotiwa kuusishwa na dalili za kichaa cha Mbwa kwa Watu walioshambuliwa
Aidha katika uzinduzi huo uliokwenda kwa kaulimbiu isemayo Kichaa cha Mbwa ‘’Wote kwa ajili ya mmoja, Afya Moja kwa wote ‘’ ziko changamoto baadhi zinaikabili Jamii kukabiliana na wimbi la ugonjwa wa kichaa cha Mbwa kama vile upatikanaji hafifu wa chanjo kwa binadamu na gharama kubwa, uwepo wa Mbwa na paka wengi wanaozurura katika miji na vijiji kumeongeza hatari kubwa.
Licha ya changamoto mbalimbali Halimashauri imejipanga kutoa elimu kwa Jamii kwa kulenga makundi na rika mbalimbali na katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo masokoni minadani na katika maeneo ya ibada pia wananchi wote hususani wamiliki wanaofuga mbwa na Paka kujitokeza kwa wingi katika vituo vya uchanjaji wa mbwa na Paka wapate chanjo ili kuwakinga na ugonjwa wa kichaa.
Zoezi la chanjo ya kichaa cha Mbwa likiendelea katika viwanja vya ujenzi Wilaya ya Liwale.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.