Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amekabidhi viti mwendo 5 kwa watu wenye mahitaji maalumu ikiwa ni lengo la kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kushirikiana na Taasisi ya Wanyamapori TAWA kupitia Pori la Akiba Selous kituo cha Liwale na Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii Tanzania Safari and Hunting.
Mheshimiwa Mlinga ameishukuru Taasisi ya Wanyamapori na wadau kwa kuendelea kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo walemavu kwani ni watu muhimu katika jamii hivyo ni muhimu kuwajali kwakuwapatia hivi viti mwendo ambavyo vitawasaidia katika shughuli mbalimbali ikiwemo za kuwaongezea kipato chao.
Aidha Mheshimiwa Mlinga” amesema kuwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya imekuwa ni kimbilio kwa watu wote wenye ulemavu hivyo kama Serikali haitaweza kuwafikia watu wote wenye mahitaji maalumu hivyo kujitokeza kwa wadau hawa muhimu hii imetusaidia sana katika kutatua changamaoto hii hapa kwetu Liwale hata hivyo natoa wito kwa makampuni mengine ya uwindaji wa kitalii yajitokeze pia ili ya weze kusaidia jamii kwa mahitaji mbalimbali”.
Kwa upande mwengine Kaimu Mkuu wa Kituo Selous Liwale Afisa Mhifadhi Sweetbert J Hayshi ameishukuru kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Tanzania Safari and Huting kwa jinsi inavyo shirikiana na TAWA katika shughuli za uhifadhi pamoja na kutoa wito kwa wakazi wa Liwale kushirikiana katika kutunza na kulinda rasilimali za wanyamapori kwa maendeleo
Hata hivyo pia amewakumbusha kuwa faida hizi zinatokana na uhifadhi na kutunza na kulinda rasilimali za wanyamapori kwani kwa kutunza tunapata makampuni ya uwindaji wa kitalii ambayo yanatuletea faida kubwa ukiachana na msaada huu wa viti mwendo ambao umetolewa na kampuni hii ya uwindaji pia Vijiji vinavyozunguka hifadhi na mapori tengefu vimeweza kupata magawio yao ya dola za kimarekani 5000 ambazo zinasaidia katika maendeleo ya vijiji ikiwemo afya, elimu pamoja na maji.
Pia Meneja wa kampuni ya Tanzania Safari and Hunting Martin John Katumbi amesema kuwa hizi ni faida za wanyamapori hivyo wanawajibu kuzirejesha kwa wananchi wenyewe ili ziwasidie katika shughuli mbalimbali hivyo amesema watendelea kutoa misaada na pia ameomba ushirikiano kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na ofisi ya Taasisi ya Wanyamapori TAWA.
Picha mbalimbali wakati Mkuu wa Wilaya akikabidhi viti mwendo kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.