Kamatia ya Fedha na Mipango ya Halimashauri ya Wilaya ya Liwale imekutana nakutembelea miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ikiwemo mradi wa nyumba ya walimu two in one katika Shule ya Sekondari Mangirikiti, mradi wa Shule ya Sekondari Kata ya Kichonda , Hospitali ya Wilaya pamoja na mradi wa Boost katika Shule ya Msingi Mbonde na jengo la utawala la Halmashauri .
Katika miradi iyo inayo tekelezwa kwa sasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya walimu two in one ambapo jumla ya shilingi milioni 95 zimetolewa kutoka Serikali kuu pia kamati ya fedha ilitembele mradi wa Shule ya Sekondari Kata ya Kichonda ambao jumla ya shilingi milioni 560 zimetolewa kutoka Serikali kuu pia miradi mingine ikiwa imekamilika na mingine ikiendelea na hatua mbalimbali za ujenzi.
Aidha kamati ya fedha imewataka wataalamu kupitia Halmashauri kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi iyo kwa ukaribu zaidi ikiwemo usimamizi wa vifaa pamoja na kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa muda walio kubaliana pia kamati imeipongeza Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi .
moja ya mradi wa nyumba za walimu two in one katika shule ya Sekondari Mangirikiti
Mradi wa shule ya Sekondari ya Kichonda ukiwa unaendelea na ujenzi katika hatua mbalimbali.
mrad
moja ya madarasa ya mradi wa boost katika shule ya msingi Mbonde.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.