Katibu Tawala wa Wilaya ya Liwale Bi Azilongwa Mwinyimvua Bohari amefungua kikao cha ufunguzi wa msimu wa zao la korosho katika katika ghala la Umoja akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ambapo katika kikao hicho ambacho kimehudhuruwi na wajumbe mbalimbali wakiwemo wajumbe wa vyombo vya ulinzi na usalama, waafisa ugani, viongozi wa vyama vya msingi pamoja na maafisa kilimo na pia maafisa Ushirika.
Katika kikao hicho Bi Bohari amewataka viongozi wa vyama vya msingi kuhakikisha wanakuwa waadilifu na kusimamia sheria na miongozo inayo wataka ili kuhakikisha wakulima wananufaika na kuacha kufanya mambo ya hovyo ikiwemo kuwadhulumu wakulima na kuwacheleweshea malipo yao bila sababu za msingi Serikali haipo tiyari kuona mkulima ananynyasika na hivyo tutawashughulikia viongozi wote wa vyama vya msingi atakaye fanya hivyo.
Pia Bi Bohari amewataka viongozi wa vyama vya msingi kuwa na vikao vya tathimini kila baada ya msimu ilikujua matatizo yanaanzaia wapi ili yawezekurekebishwa na pia kuangalia sifa za kiongozi kabla ajaajiriwa katika vyama vya msingi pia kwa upande mwingine amewasisitizia maafisa ugani kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi hususa katika vijiji ili wawe na uwelewa mpana katika kuchambua korosho na kujua mchakato mzima unaendaje mpka mzigo kufika ghalani.
Aidha amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwa makini katika msimu huu wa korosho kuhakikisha wanapambana na wale wote wenyenia ya kuwaibia wakulima au kuwadhulumu hivyo sheria itachukua mkondo wake kwa kiongozi yeyote atakaye fanya hivyo kwani baadhi ya viongozi wengi wa vyama vya msingi wamekuwa na matukio hayo na pia amewambia wakulima wote kuwa ofisi ya Mkuu w Wilaya iko wazi kwa mkulima yeyote atakaye dhulumiwa afike ofisini.
Kwa upande mwingine Bi Bohari amewakumbusha watumishi wote hususa maafisa kilimo pamoja na maafisa ugani kuwa wanathamini michango na tozo ambazo wanakatwa wakulima kuwa ndizo zimekuwa zikileta maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu na kwingineko kote pia amekitaka chama kikuu Runali kuhakikisha kinasimamia vyama vya msingi ili viweze kutekeleza majukumu yake na pia kwenye vyama vya msingi atakaye fanya kosa lolote lile la kufoji nyaraka au udanganyifu na kusababisha hasara basi atashtakiwa na kushughulikiwa yeye mwenywe na sio chama na atalipa gharama zote.
Aidha vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya ya Liwale vimewakumbusha viongozi wote wa vyama vya msingi, maafisa ugani na makarani kuhakikisha wanatimiza majukumu yao na kuacha kufanya vitendo vya udanganyifu au kudhulumu, na kuchelewesha malipo kwa wakulima basi ajue atashughulikiwa kikamilifu bali wakafanye kazi zao kwa umakini ili tuweze kujenga taifa letu kwa pamoja.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.