Katibu Tawala wa Wilaya ya Liwale Azilongwa Mwinyimvua Bohari amefungua jengo la Zahanati ya kijiji cha Turuki kata ya Mihumo lenye thamani ya shilingi milioni 121,025,500 ikiwa ni mapato ya ndani, Halmashauri ya wilaya pamoja na Serikali Kuu.
Ambapo mchanganuo wa mapato ya kijiji ya ndani yatokanayo na misitu ni Tshs 61,025,500 pato kutoka Halmashauri ya Wilaya 10,000,000 na pato kutoka serikali kuu ni 50,000,000 ambayo ya mekamilisha ujenzi huo wa zahanati ya Turuki.
Hayo yamejiri katika uzinduzi huo ulijumuhisha viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Chama Tawala pamoja na wananchi wa kijiji cha Turuki kwa kwakusherehesha na vikundi mbalimbali vya ngoma za asili pamoja na kwaya na wanamuziki wa singeli katika sherehe hiyo.
Akizungumza katika sherehe hiyo mgeni rasmi Katibu Tawala wa Wilaya baada ya kusomewa risala na jumbe tofautitofauti kupitia vikundi vya sanaa ambavyo vilipata nafasi ya kutumbuiza pamoja na maneno ya viongozi wa Kata hiyo akiwemo Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Chowe Rashid Chowe amewapongeza wananchi wa Turuki kwa kujitoa kuanzisha Zahanati kwa nguvu zao pamoja na serikali kwa kukamilisha ujenzi huo wa zahanati ambao utakwenda kutoa huduma kijijini hapo.
‘’Niwapongeze wananchi wa Turuki pamoja na viongozi wenu wa kijiji na Kata kwa kuwa pamoja kwenye ujenzi huu wa Zahanati, najuwa kuna changamoto ya maji na tembo ivyo niwaombe kuchukua taadhari zote ambazo zinaelezwa ikiwemo na zajadi na kuusiana na maji Serikali imetenga bilioni 5 kwaajili ya kuchimba visima na kumaliza tatizo hilo lakini pia tutaongeza watumishi ili kukizi mahitaji’’
Aidha Ndugu Bohari Pia amewaomba wananchi kuishi vizuri na muhudumu wa Afya ambae yuko kituoni hapo na kuwataka kuvitumia vizuri vipaji ambavyo wakonavyo kama vilivyooneshwa, lakini pia akampongeza Rais Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya kuijenga Tanzania.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya Daktari Glory Endrw akusita kuwasisitiza wamama wajawazito kuwahi kliniki na watoto wakapate chanjo’’Akina mama nawasisitiza kuwai kiliniki pale ambapo unakuwa na ujauzito ili kumnusuru Mtoto na Mama na kuepusha vifo vya mama na Mtoto pia Watoto wakapatiwe chanjo ili kujikinga na magonjwa kama vile suruwa, tetekuwanga na mengineyo’’
Hata hivyo Diwani wa kata ya Mihumo ameushukuru uwongozi wote wa Wilaya chini ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale Goodlick Mlinga pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Tina Sekambo kwa juhudi zao ambazo zimesaidia kumaliza jengo hili ambalo litahudumia zaidi ya wakazi 955 wa Turuki na leo tunafuraha kubwa kuona Turuki kuna zahanati maana niliwaaidi wakati nakuja kuomba kura 2020 na nimetimiza ahadi yangu na kutimiza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.