Katibu Tawala wa Wilaya ya Liwale ndugu Bi Azilongwa Mwinyimvua Bohari amehitimisha kilele cha siku ya Walimu duniani ambapo shamrashamra hizo zimefanyika katika uwanja wa Shule ya msingi Kambarage kwa kupambwa na maandamano na michezo mbalimbali ikiwemo kufukuza kuku, kuruka kamba pamoja mpira wa miguu.
Bi Bohari amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanoyoifanya ya kuhakikisha wanawafundisha watoto wetu na kuibua vipaji vyao ambavyo wengi wetu tulipo hapa ni jitihada za walimu wetu hivyo hatuna budi kuwashukuru na pia katika siku hii ya leo ni vyema pia tukakumbushana majukumu yetu ya msingi kama walimu.
Bi Bohari amewataka walimu kuendelea kuwa walezi wa watoto wetu kwani muda mwingi wamekuwa wakishinda na watoto wetu siku nzima na kuwafundisha hivyo ni vyema na tunajivunia kuwa na walimu ambao wanathamini kazi zao kwani kumekuwa na walimu waadilifu ambao wanatimiza majukumu yao na wapo ambao wanatabia za ovyo ikiwemo ulevi na hata matendo ya hovyo kama vile kuwataka watoto kingono hivyo tunawataka walimu hawa wabadilike.
Hata hivyo Serikali bado iko pamoja na nyie walimu katika kuhakikisha inaboresha maisha ya mwalimu imekuwa inajenga nyumba za watumishi hususa nyumba za walimu katika maeneo tofauti tofuti ili tu kuhakikisha mwalimu anapata sehemu nzuri ya kuishi na pia Serikali inaendelea kuboresha madarasa na kujenga Shule mpya nyingi ili kuhakikisha walimu wanakuwa na mazingira mazuri ya kufundishia watoto wetu.
Kwa upande wa changamoto zinazo wakabili walimu bado Serikali imeendelea kuyafanyia kazi na pia imekuwa ikajiri walimu kila mwaka ili kuhakikisha changamoto ya uhaba wa walimu inapungua katika Wilaya yetu hata hivyo Katibu Tawala Bi Bohari amewataka walimu kuachana mikopo kausha damu au kuchukua mikopo siyokuwa natija jambo linalopelekea mwalimu kuishi kwa shida na mateso hivyo tuombe taasisi za kifedha ziwe zinatupa elimu kabla ya kukopa na pia tujue je kuna umuhimu wa kukopa na chama cha walimu CWT kina jukumu la kusaidia walimu kuondokana na hili jambo.
picha za matukio mbalimbali katika siku ya kuhitimisha siku ya walimu duniani.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.