Wilaya ya Liwale kupatiwa mabomu baridi 700 kwa ajili ya kupambana na wanyama waharibufu na wakali tembo ambao wamekuwa wakiharibu mazao na kuhatarisha maisha ya watu hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dustun Kitandula (MB) wakati ikihutubia katika mkutano wa hadhara viwanja vya Nanjinji Liwale Mjini.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dustun Kitandula amefanya ziara katika Wilaya ya Liwale na kuanza kwa kufanya kikao cha ndani cha watendaji na badae kuongea na wananchi wa Liwale ambapo amewaeleza nia ya Serikali katika kupambana na wanyamapori ambao ni waharibifu tembo ikiwemo kuleta mabomu baridi 700 ambayo yatasaidia kupambana na tembo Na kutoa mafunzo mbalimbali na kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuzuia tembo.
Mheshemiwa Kitandula amesemakuwa Serikali kupitia Wizara umeunda mpango aikiwemo kuhakikisha Wilaya ya Liwale inaangaliwa kwa jicho la utaofauti ikiwemo kuongeza vifaa mbalimbali ikiwemo ndege nyuki, kuwafunga kola za kidigitali tembo ambao wapo kwenye makundi ili kuweza kufatilia nyendo zao na pia kuongeza idadi ya vijana ambao watapatiwa mafunzo ya kukabiliana na tembo katika vijiji vyao kwa sababu eneo la Wilaya ya Liwale ni kubwa na changamoto ni kubwa.
Mheshimiwa Kitandula ameendelea kuwasisitiza wananchi kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kupambana na wanyama hawa kwani kupitia bajeti hii ya mwaka wa fedha itihakikisha vifaa mbalimbali vita nunuliwa na kuongeza nguvu kazi katika eneo la Liwale na kutoa mbinu mbalimbali za kupambana na wanyama hawa ikiwemo kutumia matofali ya pilipili, senyenge, sauti za kukera, na diseli chafu yenye kutoa harufu njia hizi zitasaidia kupunguza wanyama hawa kuvamia maeneo ya watu hivyo ametoa wito kwa wananchi kutumia mbinu hizo.
Pia Mheshimiwa Waziri Kitandula amesema Serikali itahakikisha inachimba mabwawa katika hifadhi zote na mapori ili kuhakikisha tembo hawa wanapata maji hukohuko katika makazi yao na kucha kuja kwenye makazi ya watu na pia ametoa rai kwa wananchi kuacha kilimo cha kuhamahama kwani watu wengi wamekuwa wakilima katika hifadhi na hivyo kusababisha tembo kuhama kwenye makazi yao na pia idadi kubwa ya makundi ya Ngombe yamekuwa yakichangia kusababisha kero hii hivyo Mkuu wa Wilaya endelea kupambana na mifugo hii ili tuondoe changamoto hii.
Kwa upande mwingine wa kulipa fidia na kifuta machozi kwa waathirika wa wanyama waharibifu Mheshimiwa Waziri Kitandula amesekuwa mpaka sasa Serikali imefanikisha kurekebisha kanuni ambazo zilikuwa zinatumika kufanya tathimini na kulipa hivyo kuanzia sasa kanuni hizi zimeboreshwa na kuongezwa ukilinganisha na hapo awali na madeni yote ambayo wizara inadaiwa italipa kwa waathirika wote wa wanyama waharibifu na mazao ambayo yatakuwa yameharibiwa pia kwa upande wa Wilaya ya Liwale katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2024, watu 17 waliuawa na 3 kujeruhiwa na wanyama wakali na waharibifu ambapo kati yao watu 16 wamelipwa jumla ya Tshs 14,500,000.
Aidha katika mgogoro kati ya jumuiya Magingo na TANAPA Mheshimiwa Waziri amesema kuwa wizara itashughulikia kwa kutuma wataalamu ambao watakuja na kukagua mipaka upya na kuangalia na kisha pande zote zitakaa ili kuweza kumaliza mgogoro huu.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.